HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 29, 2021

JAJI WARIOBA AONGOZA MAHAFALI YA 38 YA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO SUA MOROGORO

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokine cha Kilimo (SUA) Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akimtunuku Shahada ya Uzamivu mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 38 ya chuo hicho yaliyofanyika jana mkoani Morogoro.

Kiongzi Rasmi wa shughuli za Mahafali ya 38 ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  Mlau Profesa Kalunde Sibuga akiongoza msafara wa Mkuu wa chuo kuingia kwenye ukumbi wa mahafali yaliyofanyika jana mkoani humo. 
 Mlau Profesa Kalunde Sibuga akitoa neno la ukaribisho wakati wa ufunguzi wa mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Mwenyekiti wa Baraza  Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othman akizungumza kwenye mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Raphael Chibunda akielezea utekeleza wa shughuli mbalimbali za chuo hicho.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Nabii Makamu Mkuu wa chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Profesa Maulid WaladMwatawala akizungumza kwenye mahafali hayo.


Mahafali yakiendelea.
Mkuu wa chuo hicho Jaji Joseph Warioba akiwatunuku  wahitimu.
Mahafali yakiendelea.
 

Na Calvin Gwabara, Morogoro


CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeitikiza maagizo ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere  ya kutambua mahitaji na kutatua changamoto mbalimbali za kilimo cha Tanzania na maisha ya wananchi hasa wa vijijini. 

Kauli hiyo imethibitishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo  Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman  wakati wa hotuba yake ya utekelezaji wa majukumu ya Chuo kwenye mahafali ya 38 ya Chuo hicho yaliyofantika kwenye Kampasi ya Edward Moringe Mkoani Morogoro. 

“Baraza la Chuo limeendelea kutekeleza majukumu kwa ufanisi,  majukumu hayo ni pamoja na kuisimamia Menejimenti ya Chuo ili itekeleze majukumu makuu ya Chuo ambayo ni kutoa mafunzo, kufanya utafiti, kutoa huduma za kitaalamu,ugani na kuzalisha mali na  Majukumu hayoyanatimiza kikamilifu agizo la Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye katika hotuba yake ya uzinduzi wa Chuo hiki mwaka 1984 alisema namnukuu “Chuo Kikuu hiki lazima kitambue mahitaji na kutatua matatizo ya kilimo cha Tanzania na maisha huko vijijini” mwisho wa kumnukuu Baba wa Taifa.”alibainisha Mhe. Chande. 

Aisha Kwa niaba ya Baraza la Chuo Jaji Mkuu Mstaafu Chande Othuman ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fedha za ruzuku na fedha za maendeleo inazotoa kwa Chuo kwani bila fedha hizo Chuo kisingeweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. 

“Hivi punde tutashuhudia wahitimu wakitunukiwa stahili zao za kitaaluma baada ya kuhitimu mafunzo yao mbalimbali, hivyo, napenda kuungana na wazazi, walezi, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa elimu katika kuwapongeza kwa dhati wahitimu wote kwa mafanikio waliyoyafikia kwa kufaulu na kuhitimu masomo yao na hivyo kustahili kutunukiwa tuzo walizofuzu.” alisema Jaji Othman Chande. 

“Mafanikio haya yamepatikana kutokana na bidii na ushirikiano wa wahitimu wenyewe, wanataaluma waliowafundisha,watumishi wote wa Chuo na wadau wengine, aidha nawapongeza na kuwashukuru wanataaluma na watumishi wengine wote wa Chuo waliowawezesha wahitimu hawa kufikia malengo yao ya kitaaluma”. 

Awali Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema Seneti ya Chuo katika Mkutano wake Maalum wa 271uliofanyika tarehe 17 Novemba, 2021, iliidhinisha kuwa katika mwaka wa masomo 2020/2021, Jumla ya wahitimu 4,044 (Wanaume 2,330 na Wanawake 1,714) walifaulu na kutimiza masharti yote ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu masomo yao katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo. 

“Kwa kutambua kwamba kusoma na kufikia hatua ya kutunikiwa cheti katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo haijawahi kuwa lelemama niombe ridhaa yako ya kuungana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo kuwapongeza kwa dhati watunukiwa wote kwa juhudi zao katika masomo ambazo zimewawezesha kufikia mafanikio waliyoyapata na ni matarajio yetu kwamba mafanikio haya yatakuwa kichocheo cha ufanisi, tija na ubunifu katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa ikiwemo kuzalisha mali na kutoa huduma bora kwa jamii na taifa kwa ujumla. alieleza Profesa Chibunda. 

Aidha amesema wanawatarajia wahitimu hao  wawe mabalozi wa kukitangaza Chuo vizuri kwa tabia na utendaji wao mzuri wa kazi lakini pia ni mategemeo ya Chuo kwamba watatumia elimu waliyopata kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu  kwa maendeleo ya nchi. 

Makamu huyo Mkuu wa Chuo amesema katika mwaka wa masomo 2021/2022 Chuo kimesajili wanafunzi 4,694 wa Shahada za Kwanza, Stashahada na Atashahada, pia Chuo kimesajili jumla ya wanafunzi 489 wa masomo ya uzamili (Umahiri na Uzamivu) hivyo kwa sasa Chuo kina jumla ya wanafunzi 14,581 kati yao wanafunzi 13,827 ni wa Shahada za Awali na 754 ni wa Shahada za Juu; Wanafunzi wa Kigeni waliopo chuoni ni 101 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Bara la Afrika. 

Pia amesema Utekelezaji wa majukumu ya Chuo  umezingatia  Mpango Mkakati wa Chuo wa mwaka 2021 - 2026 na  vilevile, Chuo kinatekeleza shughuli zake kwa kuzingatia sera, miongozo na kanuni zilizowekwa na Baraza la Chuo pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojojia. 

Akizungumzia upande wa Utafiti amesema Miradi mipya ya utafiti; Katika kipindi cha mwezi Desemba, 2020 hadi sasa, Chuo kimepata miradi mipya 40 ya utafiti yenye thamani ya shilingi 9,078,354,423.78 ambapo miradi  hiyo inafadhiliwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. 

Profesa Chibunda pia amezungumzia kupanda kwa Ubora wa Chuo kimataifa kuwa Chuo kimeendelea kufanya vizuri kwenye nyanja ya taaluma na utafiti na kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na mtandao wa ‘‘Webometric’’ Mwezi Julai, 2021 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kilishika nafasi ya 51 kwa ubora barani Afrika, na nafasi ya pili (2) kati ya Vyuo Vikuu 53 vya Tanzania. Nafasi ya Chuo imepanda kwa nafasi mbili ukilinganisha na matokeo ya Mwezi Januari 2021 ambapo SUA ilishika nafasi ya 67 kwa ubora katika Vyuo Vikuu bora Afrika. 

Pia ameongeza kuwa katika nyanja ya utafiti SUA imeshika nafasi ya kwanza kitaifa, nafasi ya 31 katika bara la Afrika kwa kupata nukuu (citations) 98,143 kwenye Google scholar citation index. 

Katika orodha ya watafiti bora Tanzania iliyotolewa na Shirika la ad scientific index SUA imefanikiwa kutoa watafiti bora 19 kati ya watafiti bora 50 Tanzania. Katika orodha hiyo mtafiti bora namba moja nchini (Prof. Rudovick Reuben Kazwala) anatoka SUA na kati ya watafiti kumi (10) bora SUA imetoa watafiti wanne (4).” alifafanua Makamu Mkuu wa Chuo. 

Aidha amesema Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ni miongoni mwa Taasisi za Elimu ya Juu nchini zitakazofaidika na Mradi wa Kuboresha Elimu ya Juu ili Kuinua Uchumi (HEET) unaofadhiliwa kwa mkopo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Benki ya Dunia.   

No comments:

Post a Comment

Pages