KATIKA kuhakikisha wanajiweka sawa kimaisha mara baada ya kustaafu, Wabunge nchini wameaswa kujifunza mbinu mbalimbali zikiwemo za biashara, kilimo na zingine za uzalishaji mali hatua ambayo pamoja na mambo mengine itawasaidia kuendelea kuinuka kimaisha na kukuza maendeleo ya Tanzania
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya ‘Yono Auction’ Stanley Kevela wakati akiwasilisha mada yake kwa wabunge na wafanyakazi wa Bunge katika semina maalumu iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wabunge hao katika masuala mbalimbali zikiwemo za fursa za kibiashara, ujasiriamali na uwekezaji
Akizungumza katika semina hiyo, Kevela ambaye pia ni Mbunge mstaafu wa Bunge hilo, amesema wabunge hao mbali na nafasi zao za uwakilishi walizonazo hivi sasa, wanapaswa kufikiria watafanya shuguli zipi mara watakapostaafu kazi hiyo akisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo.
Amesema ili kufikia malengo yao hususani katika nyanja za kibiashara, uwekezaji na ujasiriamali, wabunge wanapaswa kujifunza maarifa za kutoka kwa watu mbalimbali waliofanikiwa sambamba na kuhudhuria mikutano ya kibiashara na mitandao ya kijamii mfano facebook, LinkedIn, whatsapp, instagram ili kupata mbinu zaidi.
“Nipo kwenye mitandao wa wafanyabiashara duniani wenye Makao makuu yake Paris nchini Ufaransa, Nimefanya semina na mafunzo mbalimbali nchini Italy, India ,China ,Japan na Afrika Kusini kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji, hizi zote ni njia za kujifunza na kupata ujuzi ambao kama utazingatia utakupa manufaa yatakayokusaidia kuendesha maisha hapo baadae” amesema Kevela
Mbali na hilo amesema ili kufikia malengo hayo, wanapaswa kuwa na mtazamo wenye mafanikio (Chanya) na kepukana na mawazo ya kujikatisha tamaa au kukatishwa tam ana badala yake wanatakiwa kuchukulia changamoto zozote wanazokutana nazo kama sehemu ya kujifunza.
“Unapaswa kuiiamini ya kuwa una uwezo wa kufanya biashara,usisubiri subiri pale unapopata fursa bali anza mara moja, usifikirie kuwa utafanyaje pindi ukipata changamoto njiani bali jipe moyo ya kuwa hakuna jambo lisilo na changamoto, jipe moyo wakati wote kuwa utazishinda changamoto na kusonga mbele” amesisitiza Kevela wakati wa semina hiyo.
Aidha amesema yeye kama Mbunge mstaafu katika muda ambao amekuwa nje ya Bunge hilo mbali na kumiliki kampuni ya udalali ya Yono, ameweza kufanya uwekezaji katika maeneo tofauti ikiwemo kuanzisha kituo cha Redio cha Ice Fm kilichopo Makambako, Mkoani Njombe lakini pia akimiliki biashara zingine anazosema mbali na kumpatia faida zimesaidia kutoa ajira.
No comments:
Post a Comment