HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2021

KYERWA WATAKIWA KULIENZI SOKO LA NDIZI

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Rashid Mohamed Mwaimu akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani .
Baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao hicho.
 

 

Na Lydia Lugakila, Bukoba

 

Wananchi wilayani Kyerwa mkoani Kagera wametakiwa kulienzi soko la ndizi la kimataifa lililopo Kata ya Murongo wilayani humo kutokana na soko hilo kuchangia pakubwa kupatikana kwa bei nzuri kwa wakulima.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Kyerwa Rashid Mohamed Mwaimu katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Rweru plaza.

ili kuhakikisha soko hilo la kimataifa la ndizi linafanya vizuri linatakiwa kuboreshwa kwa miundo mbinu ili kuwavutia wawekezaji kutoka nje ya nchi huku akimuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo James John kuhakikisha anahimalisha soko hilo mahali lilipo soko la kimkakati huku akieleza mafanikio ya soko hilo kuwa awali mkungu mmoja wa ndizi uliuzwa kwa shilingi elfu 3,000 na Sasa ni 10,000 kwa mkungu mmoja.

"Natoa maelekezo kwa mkurugenzi hakikisha soko la ndizi Murongo linapelekwa kwenye soko la kimkakati na  ijengwe miundombinu ya  soko ambapo mazao yote ikiwemo maharage, Mahindi na ndizi yatauzwa  pale ili wageni toka mataifa ya nje wafike kununua ili kuongeza kipato kwa halmashauri yetu"alisema Rashid Mwaimu.

Mkuu huyo wa wilaya amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuanzisha mnada wa kisasa wa  mifugo kujengwa wilayani humo kwa ajili ya kuongeza kipato.

Hata hivyo amewaagiza watumishi wa halmashauri hiyo kusimamia miradi mbali mbali inayotekelezwa ili imakizike kwa wakati ikiwemo kuanza kujengwa kwa stendi ya magari Nkwenda kuimalisha soko la Rwenkolongo huku akiahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa wilaya hiyo ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ili  kuweka ulinzi wa kutosha katika soko hilo la kimataifa.

Amehimiza viongozi wilayani humo kuhakikisha miradi hiyo inamalizika kwa wakati Kufuatia agizo  la mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge aliyeagiza miradi  mbali mbali inayotekezwa ikiwemo madarasa kumalizika ifikapo  Novemba 30 mwaka huu ili kuruhusu watoto kuanza shule bila vikwazo mwezi januari mwaka 2022.

Hata hivyo mkuu wa wilaya amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kusimamia shule 3 zilizoanza kujengwa mwaka 2020 ikiwemo Bugara, Kakanja na Rwabere sekondali kumalizika kwa wakati na kupata usajili ili kupunguza mwendo mrefu kwa watoto huku lengo mahususi likiwa ni kuwezesha kila kata kuwa na shule moja ya sekondari.

No comments:

Post a Comment

Pages