HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 17, 2021

Marie Stopes wasogeza huduma mtaa Ghana, Mwanza


Na Mwandishi Wetu

 
SHIRIKA la Marie Stopes Tanzania (MST), linaloshughulikia afya hasa ya uzazi na afya kwa ujumla lImehamishia ofisi zake mtaa wa Ghana mkabala na jengo la Rock City Mall jijini Mwanza.

Taarifa ya Meneja wa Mawasiliano wa taasisi ya Marie Stopes Tanzania, Esther Shedafa imeeleza kwamba, sababu ya kuhamisha ofisi za shirika hilo kutoka Nyegezi hadi katikati ya jiji la Mwanza ni kuwafikia watanzania wa rika, rangi, kabila na hali zote kwa urahisi zaidi.

Taarifa hiyo imetoka leo Novemba 15,2021 wakati wa ufunguzi na uzinduzi wa zahanati hiyo kwenye mtaa wa Ghana.

Meneja Shedafa amebainisha kwamba miongoni mwa huduma zilizoongezwa kwenye kituo hicho ni mawasiliano ya bure kati ya mtoa na mpokea huduma za afya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, MST inaunga mkono jitihada za serikali upande wa utoaji huduma za afya ambapo wameongeza wigo wa uwepo wa madaktari bingwa wa watoto na wanawake.

“Mpaka sasa MST tunazo zahanati tisa maeneo ya Unguja Zanzibar, Musoma, Kahama, Mwanza, Mbeya, Iringa, Kimara, Arusha na hivi karibuni tunapeleka huduma hizi Makambako.

“Kwa Tanzania tunayo hospitali maalum ya mama na mtoto iliyopo Mwenge Mkoa wa Dar es Salaam, inatoa pia huduma nyingine zote za afya,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Imeeleza kwamba uongozi wa MST unawakaribisha wateja walioribu na ofisi hizo na kuwaahidi kupata huduma bora za kitabibu na kibingwa.

No comments:

Post a Comment

Pages