HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 26, 2021

Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kongamano la Wahandisi jijini Arusha


Rais wa Taasisi ya  Wahandisi (IET), Mhandisi Riziwan Qadri akizungumza na waandishi wa habari.


Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam


TAASISI ya Waandisi Tanzabia (IET), inatarajiwa kufanya kongamano la 31 la kitaifa lenye lengo la  kujadili jukumu la Uhandisi katika kutikisa mwelekeo wa maendeleo ya Taifa kupitia ukuaji wa viwanda kwa uchumi wa kati.



Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Rais wa IET, Mhandisi Riziwan Qadri amesema katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Hassan Suluhu ambalo litafanyika Disemba 2 hadi 4 jijini Arusha.


Amesema baada ya kongamano hilo wanatarajia wahandisi na mafundi kuja na njia madhubuti za kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia viwanda kwa maendeleo endelevu.


" Sote tunaona jinsi serikali yetu makini inavyotekeleza miradi ya kimkakati. Hivyo hatuna budi kuweka nguvu zetu ilii kukamilisha ujuenzi huu unao endelea kwa kulipa kodi sahihi pamoja na kubuni njia nyingine za kukuza uchumi," amesema Rais huyo.


Pia Rais huyo Mhandisi Qadri anawakaribisha wadau wote wa sekta ya ujunzi kushiriki katika kongamano hilo.


Naye Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi amesema katika kongamano hilo wataongelea miaka 60 ya sekta Wahandisi nchini.


Amesema wakati nchi inapata uhuru mwaka 1961 walikuwa na Wahandisi wawili ambapo hadi sasa wanawahandisi 32145.


Msajili huyo Mhandisi Barozi ameongeza kuwa kama nchi imejitosheleza kwa Wahandisi  na kwamba watatumia kongamano hilo kujadili ni jinsi gani  Wahandisi Watanzania wanaweza kushiriki katika mkakati wa serikali wa viwanda ili kuendelea kuleta maendeleo.


" Pua tutakuwa na kiapo cha wahandisi zaidi ya 150 watakula kiapo hiki cha utii wa taaluma ili kuweza kuonesha utii wao kwenye taaluma hii. Endapo mhandisi ataenda kinyume atachukuliwa hatua na vyombo vya sheria," amesema Mhandisi Barozi.


Kwa upande Mwenyekiti wa Kitengo cha Wahandisi wanawake ( Women chapter),kutoka IET  Mhandisi Upendo Haule amesema jamii inajua wanawake wahandisi sio fani yao.


Ameongeza kwenye kongamano hilo ambalo linajumuisha Wahandisi zaidi 1000 na wahandisi wanawake watakuwepo.


"Lengo la kuwepo kwenye kongamano hili ni kuonesha nini tunafanya, nini mchango wetu kwenye maendeleo ya Taifa letu," anesema Haule.


Mwenyekiti huyo wa Women chapter aneongeza kuwa watakuwa na banca ambalo litaonesha kazi zao za uhandisi  wanawake nini wanafanya.


No comments:

Post a Comment

Pages