Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani Suzana Raymond akizungumza na waandishi wa habari.
NA VICTOR MASANGU, PWANI
MKUU
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani
Suzana Raymond amewaonya wanaojihusisha na Rushwa kwenye miradi ya
maendeleo kuacha mara moja kwani Taasisi hiyo haitawavumilia kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria.
Suzana
ametoa onyo hilo jana alipokuwa akizingumza na waandishi wa habari
ambapo alitoa taarifa ya miezi mitatu ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo.
Alisema
TAKUKURU itakuwa macho muda wote kuhakikisha miradi ya maendeleo
inatekelezeka kwa kiwango kinachotakiwa kwani ndio njia sahihi ya
kumsaidia mwananchi kupata huduma za kijamii.
"
Tutahakikisha ukaguzi wa miradi unafanyika kila wakati kuwabaini wote
wwnyw lengo ovu, niwaombe wana Pwani msisite kutoa taarifa za vitendo
vya Rushwa kwenye miradi ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria kwa
wakati" alisema.
Alisema
TAKUKURU itaendelea kufuatilia fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya
maendeleo kwa lengo la kudhibiti ubadhilifu na pale itakapobainika
wahusika watachukuliwa hatua.
Alieleza
kuwa Taasisi hiyo itaendelea kuelimisha Umma kuhusiana na madhara ya
Rushwa ili waifahamu nafasi yao katkka mapambano ya Rushwa kwani vita
hiyo ni ya Watanzania wote.
Suzana pia alisema utafanyika utafiti katika vyuo vilivyopo kwenye mkoa huo kuona visababishi vya Rushwa ya ngono.
Alisema
wataendelea kuanzisha klabu za wapinga Rushwa shuleni ili elimu hiyo
ianzie ngazi za chini na kuandaa kizazi kinachopambana na vitendo vya
Rushwa.
No comments:
Post a Comment