Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limepokea taarifa ya kifo cha mtu ambaye tarehe 11 Mei, 2026 saa 04 :30 Asubuhi mwili wake ulikutwa kwenye maji eneo la daraja la Salender Ilala na mwili huo ambao haukuwa na jeraha lolote.
Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa wa mwili huo ni wa mtu aitwaye Aisha Miraji mkazi wa Nzasa Temeke ambaye tarehe 10 Mei, 2026 wakati akiwa na wazazi wake anapatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili kwa maradhi ambayo kwa muda tofauti tofauti katika miaka mitano yalikuwa yanamsumbua, aliwapotea akiwa eneo hilo la Muhimbili mpaka mwili wake ulipokutwa tarehe na eneo lililotajwa hapo juu.
Wazazi wake marehemu wamezielezea changamoto za kiafya za mtoto wao alizokuwa anazipitia, hata hivyo Polisi wanachunguza taarifa hiyo.





No comments:
Post a Comment