NA MWANDISHI WETU
Kuna namna nyingi za uwekezaji, kilimo, misitu, madini, uvuvi, masoko ya fedha na mitaji hii ni mifano michache tu. Kupitia halaiki wawekezaji na makampuni wanaweza waka changisha pesa kutoka watakao jitokeza kutoka kwenye jamii kwa ajili kufanya biashara, au kampeni dhidi ya jambo fulani, au mradi fulani. Cha muhimu hapa ni kwamba mtaji utatoka kutoka kwa jamii na huu mtaji unakuwa kwa ajili ya lengo fulani.
Wachangiaji wa mtaji, watapata riba, au watakuwa wamiliki wa mradi, au watakuwa sehemu ya mradi. Au hawatapata chochote zaidi ya kutambulika na heshima kutoka kwa jamii ambayo michango yao imetumikia katika hili la mwisho ina maana mchangiaji alitoa kama msaada. Kwa hiyo uchangiaji unaweza ukawa kwa sababu ya faida za kiuchumi au misaada ya bure kwa ajili ya maendeleo.
Kuna mambo makubwa matatu; wachangiaji ni wengi, ni lazima kuwe na daraja litakalo kutanisha wenye kutoa na wenye kupokea pesa, na ni lazima kuwe na tamko lililo wazi la kutaka watu washiriki kwenye uwekezaji wa namna hii.
Mwisho wa siku ni kuwa huu ni mfumo ambao waliokusanya pesa kwa namna moja au nyingine watakutana au wanakutanishwa kupitia kwa msimamizi na wanao hitaji hizo pesa kwa makubaliano maalumu.
Kimsingi kunakuwa wito na pengine ushawishi kwa jamii kushiriki kwenye kuchangia pesa kwa ajili ya dhumuni fulani kama vile kuwekeza pamoja ili kupata manufaa fulanina zaidi ikiwa faida.
Uwekezaji wa pamoja kwenye mifuko ya uwekezaji huwa na tabia kama hii lakini hapa watu wanaweka kwa masharti husika na kwa madhumuni ya kupata faidi. Wawekezaji wanawekeza wakizingatia usalama, ukwasi na faida.
Kwenye uwekezaji wa pamoja, wenye pesa watatoa watampa meneja azisimamie kwenye uwekezaji, meneja atawekeza sehemu zilizo ainishwa ikiwa ni aidha kwenye baadhi ya kampuni zilizo orodheshwa kwenye soko la hisa la dar es salaam, au kampuni binafsi yenye uhitaji na pia kukopesha benki kama akaunti za muda maalumu, pia kukopesha serakali kupitia hati fungani za muda mfupi na zile za muda mrefu.
Kama ilivyo ainishwa hapo juu, ina maana meneja atawekeza kupitia kampuni zilizo orodheshwa kwenye soko la hisa
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa ajili ya uwekezaji kwenye kukopesha hapa fedha zinakusanywa kwa madhumuni ya uwekezaji kwenye kukopesha tu, kabla ya kukopesha mambo mengi yatafanyiwa tathmini ikiwemo uwezo wa mkopaji kulipa, uaminifu wa mkopaji, historia ya mkopaji, muda wa mkopo, riba, na kama kuna mashaka yoyete kwa mkopaji na mwenendo wa uchumi wa wakati wa kukopesha na matarajio ya baadae. Hili ni jambo ambalo linafanyika kwa kufuata utaalamu na kanuni mahsusi kwa uwekezaji wa namna hii.
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja kama mfuko wa wa Ukwasi na ule wa Hati Fungani yote inayo simamiwa na UTT AMIS ni mfuko ambayo imekuwa ikitoa faida nzuri kwa wawekezaji na pia ni mifano mizuri kama chombo cha serekali ambacho kupitia uwekezaji wa pamoja hukusanya pesa kutoka kwa jumuia kwa madhumuni ya kuzikopesha kwenye sehemu tathiminiwa kwa uhakika wa kiasi kikubwa huku faida nzuri ikipatikana.
Waswahili wanasema ‘maneno matupu hayavunji mfupa’ hivyo basi kuthibitisha faida kwenye mfuko wa ukwasi tuchukulie mfano huu. Dr. Mwekezaji na Profesa Jenga wote wali staafu wakati mmoja 2013 na wote wakalipwa mafao ya shilingi milioni 100.
Profesor Jenga akaamua kununua kiwanja kwa shilingi milioni 15 na akajenga nyumba nyumba ya shilingi milioni 55 kibaha Mlandege. Na akabaki na shilingi milioni 30 ambazo alijenga banda la kuku na kuanza ufugaji. Nyumba yake angeamua kupangisha ingempa laki 250,000-300,000 kwa mwezi. Baada ya maendeleo mazuri mwaka wa pili kuku walipatwa na kideli na robo tatu wakapotea, kabla ya kideli ilibidi siku zingine aamke usiku kuongezea maji, kama ni wakati wa baridi ushushe magunia na kuwasha jiko la mkaa ili kuleta joto, na kila mara ni lazima aingie na kutoka kwenye band la kuku.
Dr. Mwekezaji yeye aliziwekeza hela zake UTT AMIS akaendelea na shughuli zake zingine baada ya miaka saba shilingi milioni 100 zake zikawa zimekuwa mpaka kufiki shilingi milioni 295. Aka chukuwa shilingi milioni 120 akaenda jenga nyumba huku akibaki na shilingi 175. Yaani Dr. Mwekezaji kawekeza UTT na kapata nyumba nzuri Zaidi na pesa Zaidi. Miaka 7 si mingi mvumilivu hula mbivu, na baada ya kuwekeza UTT hakuwa na tafrani zozote zile aliendelea na shughuli zake za kila siku huku UTT AMIS wakimfanyia kazi. Kwa maneno mengine pia alia cha pesa zake zimfanyie kazi.
Na kwa wawekezaji wa kawaida basi kwa mfuko huu wataanza na kianzio cha shilingi laki moja ( Shs 100,000) na kuongeza kuanzia shilingi elfu kumi (elfu10).
Pia kuna mifuko ya uwekezaji wa pamoja yenye kuwekeza kwenye hisa kwa hapa kwetu kampuni zilizo orodheswa kwenye soko la hisa la Dar es salaam. Mifuko inayowekeza kwenye hisa ni mifuko ambayo inaweza lipa sana kama meneja anaye simamia uwekezaji atakuwa amewekeza kwenye kampuni ambazo zina ufanisi wa hali ya juu unaopelekea kampuni hizo kupata faida nzuri. Hisa zinalipa sana haswa pale mwekezaji anapokuwa hana haraka ili kuzipa nafasi ya kukabiliana na changamoto za kupanda na kushuka aidha kwa kampuni fulani au kwa soko lote la hisa.
Kimsingi uwekezaji kwenye hisa kama uwekezaji kwenye sehemu nyingine unahitaji utaalamu na wakati mwingine uvumilivu ni muhimu sana. Hisa zina panda na kushuka au tunasema mwendo wake unategemea pamoja na mambo mengine mwendo wa soko.
Hapa nchini hatuna mfuko unao wekeza kwenye hisa peke yake. Tuna mifuko inayowekeza mchanganyiko wa kwenye hisa na kwenye ili kupata faida ya soko la hisa na mitaji basi mwekezaji anaweza chagua mfuko wenye mchanganyiko. Yani kwa aslimia fulani unawekeza kwenye hisa, na asilimia nyingine kwenye mabenki na kwenye hati fungani. Kwa kufanya hivi tunasema mwekezaji ametawanya athari za uwekezaji, kwa kupitia uwekezaji anuai yaani hajaweka mayayi yote kwenye kapu moja.
Uwekezaji wa pamoja si jambo jipya tena hapa Tanzania, kwani umedumu zaidi ya miaka 15, na walio thubutu wamefaidi kwa namna tofauti zikiwemo kukuza mtaji, kupata gawiwo la mara kwa mara, elimu na huduma mbali mbali kwa watoto, bima pamoja na ukwasi mzuri, akiba inayokuwa huku ukipata pesa zako ndani ya siku chache punde unapo zihitaji.
Faida hizi zinategemea malengo ya mwekezaji ambayo ndiyo yanapekea uchaguzi wa mfuko gani autumie katika safari yake ya uwekezaji. Lengo kuu la uwekezaji wa pamoja ni kuongeza kipato kwa mwekezaji kwa kuwekeza sehemu mbali mbali, hususani katika masoko ya mitaji na amana mbali mbali.
Mwekezaji anaweza kuanza kuwekeza mara tu baada ya mfuko mpya kuanzishwa na mara kwa mara baada ya hapo, na pia anaweza kuwekeza kwenye mifuko ambayo ipo tangia utaratibu huu kuanza kutumuika nchini Tanzania 2005. Siri ni ukishawekeza endelea kuwekeza kila mara kadri unavyoweza. Ili kuwekeza mwekezaji ni lazima afungue akaunti ya uwekezaji kwa njia ya simu *150*82#, au kutembelea ofisi za UTT AMIS.
Uwekezaji wa pamoja una faida nyingi, kama vile utaalamu wa meneja,kutawanya athari za uwekezaji, uwazi, gharama nafuu, ukwasi na unafuu wa kodi, tukisema gharama nafuu ina maana huhutaji fremu au duka, wafanya kazi, na gharama zingine kama vile za mali ghafi na mitambo mbali mbali. Uwekezaji wa pamoja unasimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania ili kumlinda mwekezaji, ikiwa na mantiki ya kuzuia kutoa machapisho yenye utata au yasiyo na tahadhari husika, kuondoa utata katika kutoa thamani ya mifuko na vipande na mambo mengine kem kem. Pia kuna mwangalizi, mkaguzi wa mahesabu na wadau wengine muhimu ili kuwa na utawala bora ambao unahakikisha haki, misingi na kanuni zinafuatwa.
Kwa kuanzisha UTT, serekali imewezesha watanzania wengi kukuza mitaji yao, kupata ajira jira, faida nyingine ni kuleta namana mbadala ya uwekezajia ambayo inavuta wawekezaji wenye kipato kikubwa na kidogo kuweka nguvu pamoja huku kipato kwa serekali kupitia kodi kikipatikana.
Jukumu kubwa la Meneja wa mfuko, mfano UTT AMIS ni kununua na kuuza vipande, kukokotoa thamani ya vipande kila siku na kuweka kwenye machapisho mbali mbali, na majukumu mengine kama ya kutoa elimu, na ya kiofisi kiujumla.
Vipande ni kama hisa lakini kuna tofauti kidogo, kwa maneno mengine mwenye vipande ni sehemu ya uwekezaji lakini mwenye hisa ni mmliki wa kampuni, hisa zina nunuliwa na kuuzwa kupitia dalali na huna uhakika wa kununua au kuuza kwa wakati unataka, lakini vipande vina nunuliwa na kuuzwa na meneja; tofauti ni nyingi na mwekezaji anaweza soma Makala zaidi ya hii kwenye tovuti mbali mbali au kutembelea ofisi za UTT, dalali wa masoko ya hisa na dhamana mbali mbali au hata pale kwenye uweledi mpana wa tasinia hii kama kwenye mabenki na taasisi zingine za fedha.
Meneja ni lazima awe mwangalifu kufuata kanuni husika, mfano kuhakikisha gharama za uendeshaji hazivuki kiasi kilichokubaliwa, na uwekezaji unafanyika ndani ya maeneo yaliyo kubaliwa na si vinginevyo.
Mwekezaji anaungana na wawekezaji wengine kuwekeza pamoja hivyo basi kwa umoja huo kuwa na mtaji mkubwa ambao unawezesha kufanya mambo ambayo peke yake labda asingeweza kuyafanya, na pia kuongeza nguvu na ufanisi kwenye majadiliano na huu tunaasema ni uwekezaji wenye tija, Mwkezaji anaweza kuingia na kutoka wakati wowote kutokana na masharti ya mfuko.
Wawekezaji kwenye mfuko mmoja mara nyingi huwa na lengo moja mfano waliopo kwenye mfuko wa Wekeza Maisha wanataka bima na kukuza mtaji, lakini mfuko wa Watoto yaweza kuwa elimu na maisha baada ya shule kwa watoto. Mfuko wa hati fungani na Mfuko wa Jikimu gawio la mara kwa mara, huku mfuko wa umoja kukuza mtaji huku ukitarajia hisa zitakupa zaidi, mfuko wa ukwasi walau asilimia 10 mpaka 14 au kutokana na rejesho kutoka sehemu kama vile akaunti za muda maalumu, hati fungani za mda mfupi au mrefu. Kipande kinaweza kupanda au kushuka hili ndilo angalizo kuu.
xxxxxxxxx
Kuna namna nyingi za uwekezaji, kilimo na misitu, madini, uvuvi, masoko ya fedha na mitaji hii ni mifano michache tu. Kupitia halaiki wawekezaji na makampuni wanaweza waka changisha pesa kutoka watakao jitokeza kutoka kwenye jamii kwa ajili kufanya biashara, au kampeni dhidi ya jambo fulani, au mradi fulani. Cha muhimu hapa ni kwamba mtaji utatoka kutoka kwa jamii na huu mtaji unakuwa kwa ajili ya lengo fulani.
Wachangiaji wa mtaji, watapata riba, au watakuwa wamiliki wa mradi, au watakuwa sehemu ya mradi. Au hawatapata chochote zaidi ya kutambulika na heshima kutoka kwa jamii ambayo michango yao imetumikia katika hili la mwisho ina maana mchangiaji alitoa kama msaada. Kwa hiyo uchangiaji unaweza ukawa kwa sababu ya faida za kiuchumi au misaada ya bure kwa ajili ya maendeleo.
Kuna mambo makubwa matatu; wachangiaji ni wengi, ni lazima kuwe na daraja litakalo kutanisha wenye kutoa na wenye kupokea pesa, na ni lazima kuwe na tamko lililo wazi la kutaka watu washiriki kwenye uwekezaji wa namna hii.
Mwisho wa siku ni kuwa huu ni mfumo ambao waliokusanya pesa kwa namna moja au nyingine watakutana au wanakutanishwa kupitia kwa msimamizi na wanao hitaji hizo pesa kwa makubaliano maalumu.
Kimsingi kunakuwa wito na pengine ushawishi kwa jamii kushiriki kwenye kuchangia pesa kwa ajili ya dhumuni fulani kama vile kuwekeza pamoja ili kupata manufaa fulanina zaidi ikiwa faida.
Uwekezaji wa pamoja kwenye mifuko ya uwekezaji huwa na tabia kama hii lakini hapa watu wanaweka kwa masharti husika na kwa madhumuni ya kupata faidi. Wawekezaji wanawekeza wakizingatia usalama, ukwasi na faida.
Kwenye uwekezaji wa pamoja, wenye pesa watatoa watampa meneja azisimamie kwenye uwekezaji, meneja atawekeza sehemu zilizo ainishwa ikiwa ni aidha kwenye baadhi ya kampuni zilizo orodheshwa kwenye soko la hisa la dar es salaam, au kampuni binafsi yenye uhitaji na pia kukopesha benki kama akaunti za muda maalumu, pia kukopesha serakali kupitia hati fungani za muda mfupi na zile za muda mrefu.
Kama ilivyo ainishwa hapo juu, ina maana meneja atawekeza kupitia kampuni zilizo orodheshwa kwenye soko la hisa
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa ajili ya uwekezaji kwenye kukopesha hapa fedha zinakusanywa kwa madhumuni ya uwekezaji kwenye kukopesha tu, kabla ya kukopesha mambo mengi yatafanyiwa tathmini ikiwemo uwezo wa mkopaji kulipa, uaminifu wa mkopaji, historia ya mkopaji, muda wa mkopo, riba, na kama kuna mashaka yoyete kwa mkopaji na mwenendo wa uchumi wa wakati wa kukopesha na matarajio ya baadae. Hili ni jambo ambalo linafanyika kwa kufuata utaalamu na kanuni mahsusi kwa uwekezaji wa namna hii.
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja kama mfuko wa wa Ukwasi na ule wa Hati Fungani yote inayo simamiwa na UTT AMIS ni mfuko ambayo imekuwa ikitoa faida nzuri kwa wawekezaji na pia ni mifano mizuri kama chombo cha serekali ambacho kupitia uwekezaji wa pamoja hukusanya pesa kutoka kwa jumuia kwa madhumuni ya kuzikopesha kwenye sehemu tathiminiwa kwa uhakika wa kiasi kikubwa huku faida nzuri ikipatikana.
Waswahili wanasema ‘ maneno matupu hayavunji mfupa’ hivyo basi kuthibitisha faida kwenye mfuko wa ukwasi tuchukulie mfano huu. Dr. Mwekezaji na Profesa Jenga wote wali staafu wakati mmoja 2013 na wote wakalipwa mafao ya shilingi milioni 100.
Profesor Jenga akaamua kununua kiwanja kwa shilingi milioni 15 na akajenga nyumba nyumba ya shilingi milioni 55 kibaha Mlandege. Na akabaki na shilingi milioni 30 ambazo alijenga banda la kuku na kuanza ufugaji. Nyumba yake angeamua kupangisha ingempa laki 250,000-300,000 kwa mwezi. Baada ya maendeleo mazuri mwaka wa pili kuku walipatwa na kideli na robo tatu wakapotea, kabla ya kideli ilibidi siku zingine aamke usiku kuongezea maji, kama ni wakati wa baridi ushushe magunia na kuwasha jiko la mkaa ili kuleta joto, na kila mara ni lazima aingie na kutoka kwenye band la kuku.
Dr. Mwekezaji yeye aliziwekeza hela zake UTT AMIS akaendelea na shughuli zake zingine baada ya miaka saba shilingi milioni 100 zake zikawa zimekuwa mpaka kufiki shilingi milioni 295. Aka chukuwa shilingi milioni 120 akaenda jenga nyumba huku akibaki na shilingi 175. Yaani Dr. Mwekezaji kawekeza UTT na kapata nyumba nzuri Zaidi na pesa Zaidi. Miaka 7 si mingi mvumilivu hula mbivu, na baada ya kuwekeza UTT hakuwa na tafrani zozote zile aliendelea na shughuli zake za kila siku huku UTT AMIS wakimfanyia kazi. Kwa maneno mengine pia alia cha pesa zake zimfanyie kazi.
Na kwa wawekezaji wa kawaida basi kwa mfuko huu wataanza na kianzio cha shilingi laki moja ( Shs 100,000) na kuongeza kuanzia shilingi elfu kumi (elfu10)
Pia kuna mifuko ya uwekezaji wa pamoja yenye kuwekeza kwenye hisa kwa hapa kwetu kampuni zilizo orodheswa kwenye soko la hisa la Dar es salaam. Mifuko inayowekeza kwenye hisa ni mifuko ambayo inaweza lipa sana kama meneja anaye simamia uwekezaji atakuwa amewekeza kwenye kampuni ambazo zina ufanisi wa hali ya juu unaopelekea kampuni hizo kupata faida nzuri. Hisa zinalipa sana haswa pale mwekezaji anapokuwa hana haraka ili kuzipa nafasi ya kukabiliana na changamoto za kupanda na kushuka aidha kwa kampuni fulani au kwa soko lote la hisa.
Kimsingi uwekezaji kwenye hisa kama uwekezaji kwenye sehemu nyingine unahitaji utaalamu na wakati mwingine uvumilivu ni muhimu sana. Hisa zina panda na kushuka au tunasema mwendo wake unategemea pamoja na mambo mengine mwendo wa soko.
Hapa nchini hatuna mfuko unao wekeza kwenye hisa peke yake. Tuna mifuko inayowekeza mchanganyiko wa kwenye hisa na kwenye
Ili kupata faida ya soko la hisa na mitaji basi mwekezaji anaweza chagua mfuko wenye mchanganyiko. Yani kwa aslimia fulani unawekeza kwenye hisa, na asilimia nyingine kwenye mabenki na kwenye hati fungani. Kwa kufanya hivi tunasema mwekezaji ametawanya athari za uwekezaji, kwa kupitia uwekezaji anuai yaani hajaweka mayayi yote kwenye kapu moja.
Uwekezaji wa pamoja si jambo jipya tena hapa Tanzania, kwani umedumu zaidi ya miaka 15, na walio thubutu wamefaidi kwa namna tofauti zikiwemo kukuza mtaji, kupata gawiwo la mara kwa mara, elimu na huduma mbali mbali kwa watoto, bima pamoja na ukwasi mzuri, akiba inayokuwa huku ukipata pesa zako ndani ya siku chache punde unapo zihitaji. Faida hizi zinategemea malengo ya mwekezaji ambayo ndiyo yanapekea uchaguzi wa mfuko gani autumie katika safari yake ya uwekezaji. Lengo kuu la uwekezaji wa pamoja ni kuongeza kipato kwa mwekezaji kwa kuwekeza sehemu mbali mbali, hususani katika masoko ya mitaji na amana mbali mbali.
Mwekezaji anaweza kuanza kuwekeza mara tu baada ya mfuko mpya kuanzishwa na mara kwa mara baada ya hapo, na pia anaweza kuwekeza kwenye mifuko ambayo ipo tangia utaratibu huu kuanza kutumuika nchini Tanzania 2005. Siri ni ukishawekeza endelea kuwekeza kila mara kadri unavyoweza. Ili kuwekeza mwekezaji ni lazima afungue akaunti ya uwekezaji kwa njia ya simu *150*82#, au kutembelea ofisi za UTT AMIS.
Uwekezaji wa pamoja una faida nyingi , kama vile utaalamu wa meneja,kutawanya athari za uwekezaji, uwazi, gharama nafuu, ukwasi na unafuu wa kodi, tukisema gharama nafuu ina maana huhutaji fremu au duka, wafanya kazi, na gharama zingine kama vile za mali ghafi na mitambo mbali mbali.
Uwekezaji wa pamoja unasimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania ili kumlinda mwekezaji, ikiwa na mantiki ya kuzuia kutoa machapisho yenye utata au yasiyo na tahadhari husika, kuondoa utata katika kutoa thamani ya mifuko na vipande na mambo mengine kem kem. Pia kuna mwangalizi, mkaguzi wa mahesabu na wadau wengine muhimu ili kuwa na utawala bora ambao unahakikisha haki, misingi na kanuni zinafuatwa.
Kwa kuanzisha UTT, serekali imewezesha watanzania wengi kukuza mitaji yao, kupata ajira jira, faida nyingine ni kuleta namana mbadala ya uwekezajia ambayo inavuta wawekezaji wenye kipato kikubwa na kidogo kuweka nguvu pamoja huku kipato kwa serekali kupitia kodi kikipatikana.
Jukumu kubwa la Meneja wa mfuko, mfano UTT AMIS ni kununua na kuuza vipande, kukokotoa thamani ya vipande kila siku na kuweka kwenye machapisho mbali mbali, na majukumu mengine kama ya kutoa elimu, na ya kiofisi kiujumla. Vipande ni kama hisa lakini kuna tofauti kidogo, kwa maneno mengine mwenye vipande ni sehemu ya uwekezaji lakini mwenye hisa ni mmliki wa kampuni, hisa zina nunuliwa na kuuzwa kupitia dalali na huna uhakika wa kununua au kuuza kwa wakati unataka, lakini vipande vina nunuliwa na kuuzwa na meneja; tofauti ni nyingi na mwekezaji anaweza soma Makala zaidi ya hii kwenye tovuti mbali mbali au kutembelea ofisi za UTT, dalali wa masoko ya hisa na dhamana mbali mbali au hata pale kwenye uweledi mpana wa tasinia hii kama kwenye mabenki na taasisi zingine za fedha.
Meneja ni lazima awe mwangalifu kufuata kanuni husika, mfano kuhakikisha gharama za uendeshaji hazivuki kiasi kilichokubaliwa, na uwekezaji unafanyika ndani ya maeneo yaliyo kubaliwa na si vinginevyo.
Mwekezaji anaungana na wawekezaji wengine kuwekeza pamoja hivyo basi kwa umoja huo kuwa na mtaji mkubwa ambao unawezesha kufanya mambo ambayo peke yake labda asingeweza kuyafanya, na pia kuongeza nguvu na ufanisi kwenye majadiliano na huu tunaasema ni uwekezaji wenye tija, Mwkezaji anaweza kuingia na kutoka wakati wowote kutokana na masharti ya mfuko.
wawekezaji kwenye mfuko mmoja mara nyingi huwa na lengo moja mfano waliopo kwenye mfuko wa Wekeza Maisha wanataka bima na kukuza mtaji, lakini mfuko wa Watoto yaweza kuwa elimu na maisha baada ya shule kwa watoto. Mfuko wa hati fungani na Mfuko wa Jikimu gawio la mara kwa mara, huku mfuko wa umoja kukuza mtaji huku ukitarajia hisa zitakupa zaidi, mfuko wa ukwasi walau asilimia 10 mpaka 14 au kutokana na rejesho kutoka sehemu kama vile akaunti za muda maalumu, hati fungani za mda mfupi au mrefu. Kipande kinaweza kupanda au kushuka hili ndilo angalizo kuu.
Ili kuanza kuwekeza sio lazima uwe na hela nyingi, kuanzia shilingi elfu kumi tayari unakuwa mwekezaji, siri ni kuendelea kuwekeza kwa mpango maalumu, mpango wako unaweza ukuwa wa kila siku, kila wiki, kila mwezi au kila mwaka. Kwa mfano asilimia 10 ya kila mapato yako yawe ya siku, mwezi ..kwa wale walio na mtaji mkubwa anaweza kuwekeza kwa mkupuo mkubwa lakini si vibaya wakiongeza juu ya huo mkupuo kwa mpango maalumu kwani haba na haba hujaza kibaba. Ulipaji kwa njia za mitandao mfano simu una rahisisha na kuokoa muda wa kwenda benki mara kwa mara, mwekezaji ataomba nakala ya uwekezaji wake wakati wowote na ni jukumu la meneja kumpa mwekezaji taarifa za uwekezaji wake pale anapohitaji. Mwekezaji anaweza akawa anavuna kutoka kwenye uwekezaji wake kwa mpango maalum na si lazima akitaka pesa zake atoe zote. Atatoa kutokana na mahitaji yake na muda wowote anaweza kuongeza tena uwekezaji.
Mwekezaji anaweza kujipangia alipwe kiasi fulani cha faida yake kila baada ya muda fulani, meneja atalipa kiasi hicho kwa akaunti ya mteja kwa muda muafaka, na pia si lazima kuvuna faida, anaweza acha faida na yenyewe ikawa sehemu ya uwekezeja yaani faida ikaendelea kumpa faida, akiwa na shida au mahitaji fulani, waswahili wana usemi kimfaacho mtu chake hivyo basi anaweza kutoa hela kutoka kwenye akaunti yake ya uwekezaji vile apendavyo.
Ukifanya upembuzi yakinifu, kwa haraka utakuta kuwa uwekezaji wa pamoja ni fursa nzuri kwa maisha ya mbele na mwekezaji akautumia vizuri utamsaidia kutatua changamoto mbali mbali na pengine kumsaidia kwenye maisha ya kustaafu kwani wakati wa kustafuu ni kama una anza ukurasa mpya na wakati huo pesa ndiyo zinahitajika kwa wingi, hivyo basi uwekezaji wa pamoja unaweza kuwa kama pensheni mbadala au hata zaidi ya pensheni.
Mwekezaji lazima awe na malengo mfano lini avune, apande mbegu mara kwa mara au mara moja, haya ni malengo ya kawaida kwenye biashara yeyote ile.
Mwekezaji ni mtu mwerevu anatakiwa afanye tathmini ya athari zinazoweza tokana na uwekezaji huu, na sababu zipi ninafanya kipande kupanda au kushuka. Ni muhimu pia mwekezaji kumfanyia upembuzi meneja kwani huyu ndiye baada ya makubaliano maalumu na ya kisheria utampa pesa zako awekeze kwa niaba yako, huku ukiendelea na shughuli nyingine. Na meneja utamjuwa anaweza au hawezi kwa kuangalia utendeji wake, mfano je anafikia malengo na vigezo vilivyowekwa na anavizidi kwa kwa kiasi gani? Kwa mfano kigezo kimojawapo ni asilimia ya chini ambayo mwekezaji anatarajia, je anaifikia na kuizidi kwa kiasi gani, na hii ni kila mwaka au? Vyeti vya meneja na wafanyakazi wake, walivyojipanga, utendaji wa meneja miaka 5-10 iliyopita n.k.
Kawaida akanti moja ni ya mtu mmoja, pia mnaweza fungua akaunti ya kikundi, na uwekezaji huu ni wa mtu, watu, tasisi zote wakiwemo wafanya biashara wadogo na wakubwa.
Ni rahisi na salama kwa asilimia kubwa ukilinganisha na uwekezaji mwingine wowote hii inatokana na na muundo wake, pia unatoa nafasi kwa mwekezaji kumwandika mrithi wake kama litatokea lakutokea huko mbele. Una ruhusu mlezi au mwangalizi kumwekezea mwenye umri chini ya miaka 18 na akifika wakati huo kumkabidhi kilichopo na akaamua kundeleza au kufika ukomo. Kumbuka kuwekeza na kutoa pesa ni rahisi. Ukishakuwa na akaunti unaweza ukawa unawekeza kwa simu, wakati wowote.
Chukuwa hatua, jiulize kwanini ni wekeze hii itasaidia kufanya tathimini kwa kulinganisha faida na athari za ungeamua kuwekeza sehemu nyingine mbali na kwenye uwekezaji wa pamoja. Tathimini hii iendane na malengo yako, muda, athari na faida tarajiwa.
Malengo yatakupa kigezo cha mfuko upi uwekeze, kwa kuangali mfuko husika unawekeza wapi na wapi. Mfano muda ukiwa mrefu sana mfuko wenye hisa kama sehemu yake ya uwekezaji unaweza kutumika. Ila kama ni ya muda mfupi mfuko wenye kuwekeza zaidi ya alimia 90 kwenye hati fungani utafaa zaidi. Hizi ni tathmini chache tu. Mwekezaji anashauriwa kupata elimu ya kutosha kabla ya kufanya uamuzi na elimu kama hii hutolewa bure na UTT AMIS.
Kwa maneno mengine ni vizuri watanzania wakajipanua zaidi na kufanya uwekezaji kisasa. Ukiwa huna hela nguvu zako ndiyo mtaji, kama huwezi kujiajiri ni lazima uwe mtumwa yaani uajiriwe, ukiwa na hela pesa zako zinakufanyia kazi.
Pamoja na uwekezaji wa pamoja kuna huduma kama vile usimamizi wa mali/ pesa uwekezaji wa mteja hii huduma ni nzuri na ni njia ya kisasa kwa mwekezaji kumpa msimamizi pesa zake awekeze kwa ajili yake yaani mwekezaji anampa meneja msimamizi mali, anasiamamia huku akiratibu huduma mbali mbali kama vile wapi ziwekezwe, ushauri wa kodi n.k . msimamizi hawekezi tu lakini pia anakuwa ndo bwana ushauri kwa mwekezaji huku akifanya tathimini ya hali halisi sokoni, mfano kuangalia uwezekano wa kukwepa dhoruba za uwekezaji na kuhakikisha faida zinapatikana. Yaani hapa mwekezaji anaweza kupata huduma kama usimamizi wa mali zake huku ukipata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kuongeza uwekezaji wake kwa faida.
Katika huduma yausimamizi wa mali meneja ataangalia mtawanyo wa mali za mwekezaji, bajeti ya mwekezaji, hesabu zake, kodi, na hata bima husika. Kwa sababu meneja anajuwa basi jukumu lake litakuwa kuhakikisha kuwa mali zinazoshikika na zisizo shikika zinawekezwa kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuleta mapato ya juu kabisa.
Huduma hii ya usimamizi wa mali mara nyingi unalenga mashirika kama ya pensheni na watu wenye pesa nyingi. Kwa wale wenye pesa kidogo wataanza kwenye uwekezaji wa pamoja huku wakichanganya na shughuli zao zingine ili kukuza mtaji ambao baadae utwapa uwezo wa kuingia huku.
Kwa mtu au taasisi wakichaguwa kuweka meneja, lengo ni kuwa meneja huyo ataleta tija zaidi.
Kuna mambo makubwa mawili mwekezaji anatakiwa kuyafahamu, la kwanza nafasi ya meneja kwenye uwekezaji wake na pili mikakati ya meneja kuongeza rasilimali husika.
Meneja atawekeza wapi, umuhimu wa hili ni kuwa utapata kubashiri faida au au hasara kwani kama meneja anawekeza kwenye kampuni ambazo haisimamiwi vizuri na hazina biashara ya kutosha na hivyo basi kuleta hasara.
Mikakati ya meneja kuongeza rasimali husika utaifahamu kwa kuuangali weledi wa wafanya kazi, historia ya utendejin wake wa sasa na huko ulipotoka
Lakini pia ili kujuwa kama meneja anafanya vizuri au laa, utafanya upembuzi yakinifu katika uwekezaji ambao ni linganishi, kwa mfano utafanya udadisi wa maendeleo ya vipande dhidi ya hisa, hati fungani za muda mrefu, dhidi ya akaunti za muda maalumu na pengine hata faida zinazoptaika kutokana na ardhi na majengo.
Utaangalia pia mifumu meneja anayo tumia, jinsi anaweka kumbu kumbu za mali anazo simamia, na utoaji wa taarifa za wawekezaji za kila siku.
Haya ni baadhi ya mambo muhimu tu ambayo ni muhimu kwa mwekezaji anapaswa kuyafahamu.
No comments:
Post a Comment