Prof. Norman King.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
RAIS wa Taasisi ya Wataalamu wa Utazamaji wa Uchaguzi Afrika(ANEOPI), Prof. Norman King ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Hai, Moshi amechukua fomu jana ya kuomba kuteuliwa na chama cha Mapindizi (CCM),nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kurudisha fomu hiyo King alisema lengo la kuchukua fomu hiyo ni kwa sababu ya changamoto ikiwa ni pamoja na muundo wa katiba kubadilika
King ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya za Mbeya na Songea alisema kutokana na mabadiliko hayo kunahitajika Spika mwenye ueledi mzuri wa kukielewa chama cha CCM vizuri.
"Kwa sasa ni muhimu mabadiliko yakawepo ni lazima Spika awe ni mtu mwenye ufahamu wa kutosha kuweza kukidhi hoja za wabunge," alisema King.
Aliongeza kuwa kuna watu mashuhuri waliochukua fomu na kwenye CCM watu hao wapo wengi yoyote anaweza kuwa Spika kwa kadri chama kinavyotaka.




No comments:
Post a Comment