HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 22, 2022

Lindeni Rasilimali za Bahari-Sada Mkuya

 


Na Raya Hamad – OMKR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya amesema ujenzi wa Ukuta wa mawe katika fukwe ya mwambao wa eneo la Msuka una lengo la kudhibiti athari za mmongonyoko wa fukwe hiyo.

Hayo ameyaeleza wakati alipofanya ziara ya pamoja na Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwenye fukwe za Shehia ya Msuka Magharibi mwa kisiwa cha Pemba na kushuhudia ujenzi unaoendelea wa ukuta huo

Dkt Saada amewaomba wananchi na hasa wavuvi wanaotumia eneo hilo kuhakikisha wanalinda na kutunza ukuta huo kwa maslahi yao na vizazi vijavyo pamoja na kuchukuwa tahadhari katika kulinda rasilimali za bahari na viumbe hai kwa kuepuka matumizi ya mifuko ya plastiki na kutotupa ovyo chupa za plastiki

Amewasisitiza kuwa shughuli zao za kijamii na uvuvi ziendelee bila ya kuathiri ukuta huo ambao Serikali imechukuwa jitihada kubwa katika kulinda na kuhifadhi mazingira ya eneo hilo yasiathirike pamoja na kuondoa uwezekano wa athari za kiuchumi na kijamii zilizokuwa zimejitokeza

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Mhe Hassan Hafidh ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa usimamizi mzuri uliopelekea kujengwa kwa ukuta huo uliozingatia muda na mahitaji ya wavuvi na wananchi wa eneo hilo

Nae Mhandisi Atanasi Abdul Malik Said kutoka ofisi ya wakala wa majengo amesema tayari ujenzi huo umeshafikia urefu wa mita 500 na shughuli zinazoendelea kwa sasa ni ujenzi wa nguzo na kuweka mkanda kwenye ukuta kwa ajili ya kuimarisha na kutia nguzo zaidi ya 120 kwa ukuta wote wa mita 500

Pia hatua nyengine ni kutengeneza misingi ama njia za maji ya mvua kutoka juu hadi baharini, kufukia maeneo yote ya ukuta, na kujenga ngazi za kuteremkia baharini kwa ajili ya wavuvi na wote wanaomahitaji ya eneo hilo

Akiwakilisha wavuvi na wachuuzi wa eneo hilo Bw Khamis Suleiman Amour kwa niaba ya wenziwe wameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na uongozi uliofika kwa kutimiza ahadi na kuihakikishia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa watakuwa walinzi wema wa eneo hilo ili lisiharibiwe na harakati za kibinaadamu

Kwa upande wake Bi Sara Mohamed mkulima wa mwani amesema kabla ya kujengwa ukuta huo walikuwa wakipata shida ya kutokana na kukosa eneo maalum la kuanikia mwani kwani mara nyingi mwani wao ulichukuliwa na mwani ama kukosa kiwango cha ubora lakini sasa ukuta umekuwa ni mkombozi maji hayawafikii na kuharibu mwani wao

Athari kadhaa zilikwishajitokeza kabla ya kujengwa kwa ukuta huo ikiwa ni pamoja na kupotea kwa mikoko na miti mengine, kupotea kwa viumbe hai katika maeneo ya fukwe, kuharibika kwa mashamba na kupungua kwa ardhi ya kilimo, kuwepo hatari ya kuingiliwa na maji ya bahari kwa makaburi, kupotea kwa majengo muhimu ikiwemo msikiti, kuwepo kwa tishio la kuathiriwa kwa kambi ya KMKM iliyopo eneo hilo

Katika kufanikisha kazi ya ujenzi wa ukuta huo jumla ya shilingi 300,000,000 zilipangwa kutumika ambapohadi kufikia mwezi Disemba 2021 shilingi 200,000,000, fedha zilizobakia shilingi 100.000.000.0 zitatumika kujenga ukuta kwa ajili ya kuweka uimara zaidi, mradi unategemea kumalizika mwishoni mwa mwezi wa Mach, 2022

No comments:

Post a Comment

Pages