HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2022

NIC, TIRA kwa kushirikiana na IFAD utekelezaji Sera ya Kilimo na Mifugo kuwakomboa wakulima wadogowadogo


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya NIC leo Jijini Dar es Salaam.


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Shirika  la Bima la Taifa (NIC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Mfuko wa kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) wamepanga kuanzisha Uandaaji wa Sera ya Kilimo na Mifugo ambayo itaelezea kwa kiasi kikubwa namna gani wanaweza kutekeleza Bima ya Kilimo na Biima kwa ajili ya mifugo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam mara baada y kutembelewa na Kamishna wa Bima Nchini Dkt. Baghayo Saqware, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC ,Elirehema Doriye amesema ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija na kilimo ambacho kinavutia watanzania wengi mojawapo ya vitu vya msingi ni kuhakikisha bima ya kilimo inakuwepo lakini pia sera za kilimo zinaenda kugusa wakulima wadogowadogo na kuhakikisha kwa umoja wao wanaweza wakazalisha.

“Bima ya kilimo kazi yake kubwa ni kuhakikisha inamuondolea hasara ambazo mkulima anawezapata kutokana na majanga mbalimbali kama mvua iliyozidi, wadudu ambao wanashambulia mazao , mvua za mawe, ukame na vitu vyote ambavyo vinaweza kuathiri kilimo na uzalishaji”. Amesema

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mfuko huo ,Jackline Machango amesema wameona umuhimu katika suala hilo hivyo wameamua kuweka mkono wao kuona ni namna gani wanaweza kusaidiana na TIRA pamoja na NIC kuandaa Sera hiyo ya Bima pamoja na kuitekeleza kwa kiwango ambacho kinaweza kuonekana kwa kiasi gani sera hii inaweza kufanya kazi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kuzindua ofisi mpya ya Shirika la Bima la Taifa (NIC), Kamishna wa Bima (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware ameiopongeza NIC kwa kazi ambazo wanazifanya hasa kuhakikisha wanamjali mteja kuanzia utoaji huduma pamoja na eneo la utoaji huduma.

Aidha amewataka watumishi wa NIC kuhakikisha wanaendelea kuongeza juhudi katika kazi pia kuhakikisha ofisi zote za shirika hilo zinakuwa vizuri na salama kwaajili ya utoaji huduma kwa Watanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages