HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 22, 2022

Rais Dk. Mwinyi mgeni rasmi uzinduzi wiki ya sheria

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akizungumza na waandishi wa habari.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi anatarajiwa kufanya uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Sheria utakaofanyika tarehe 23 January mwaka huu Jijini Dodoma.

Pia taasisi zote  za serikali, binafsi, makundi mbalimbali, wadau wote wa mahakama na wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma kwa ujumla na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenye sherehe hizo za maadhimisho ya wiki ya Sheria kitaifa.


Maadhimisho yatakuwa  sherehe  za uzinduzi na kwamba kuwakuwa  zoezi la matembezi yatakayoanza saa12:00 asubuhi katika viwanja vya kituo jumuishi Cha haki Jijini  Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 21 jijini Dodoma  Mkuu wa Mkoa huo, Antony Mtaka  amesema matembezi hayo yataanzia viwanja vya kituo Jumuishi Cha Haki (Jengo jipya la mahakama karibu na Hazina) na kuishia kwenye viwanja vya Nyerere square ambapo sherehe za uzinduzi zitafanyika.

Mataka amesema maadhimisho hayo  yatafanyika kwa wiki nzima yakijumuisha shughuli ya  uzinduzi wa bendera ya mahakama(Januari 23,22),uzinduzi wa Mahakama ya wilaya ya chemba (Januari 25,2022),uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la makao makuu ya mahakama ya tanzania-judicial square (Januari 26,2022) na Uzinduzi wa Mahakama ya wilaya ya bahi(January 28,2022).

Amewataka wakaziwa Mkoa wa Dodoma na jirani kujitokeza  kwa wingi katika maadhimisho ya wiki ya Sheria kitaifa yanayoanza Januari 23 hadi 29,2022 na siku ya Sheria nchini Februari 1,2022 kuungana na  Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa serikali ya Mapindizi ya Zanzibar Dk. Mwinyi.

Kwa upande wake, Naibu Msajili wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma, Benard Mpepo amesema kwenye maadhimisho hayo kutakuwa na uzinduzi wa majarida na sheria mbalimbali zinazohusu mahakama zitakazofanywa na jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

amesema Januari 23, kutakuwa na uzinduzi wa bendera ya mahakama, Januari 25 uzinduzi wa mahakama ya wilaya ya  Chemba, Januari 26 uwekaji jiwe la msingi la mradi wa jengo la makao makuu ya mahakama ya Tanzania na Januari 28 uzinduzi wa Mahakama ya wilaya ua Bahi.

Hatahivyo, sherehe za siku ya sheria nchini zitakazofanyika katika viwanja vya bustani ya chinangali Februari 1,2022 Mgeni rasmi katika sherehe hizo anatarajiwa kuwa  Rais Samia.

No comments:

Post a Comment

Pages