Jaji Mkuu wa Tanzania,Profesa Ibrahimu Juma akisaini kitabu cha wageni katika moja ya mabando ya maonesho ya wiki ya Mahakama.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
JAJI Mkuu wa Tanzania,Profesa Ibrahimu Juma amesema kuwa itakapofika Disemba 31,2025 wawe ni nchi inayoshindana na nchi yoyote ulimwenguni katika masuala ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), ya Mahakama kwa lengo la kuwasaidia wananchi utoaji wa Huduma.
Prof Juma ameyasema hayo leo Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki maonesho ya wiki ya Sheria ambayo Kitaifa yanafanyika kwenye Viwanja vya Nyerere Skwea Jijini hapo yenye kauli mbiu " Zama za Mapindizi ya nne ya Viwanda. Safari ya maboresho kuelelea Mahakama Mtandao, " amesema kuna haja ya kuboreshwa kwa mifumo mitandao.
Pia amesem mifumo ya Mahakama mtandao itawasaidia wananchi utoaji huduma na kukuza uchumi kwani mifumo mingi ya Mahakama kwa Sasa imekuwa na changamoto ya kutosoma na hivyo kutoleta manufaa kwa wananchi hao.
"Ushindani wa teknolojia tumebakisha miaka minne ya robo ya kwanza itakuwa ni jukumu la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutayarisha dira ijayo ya miaka 25 ijayo," amesema Jaji Mkuu.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo akiwemo Afisa Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamabana na Rushwa (TAKUKURU),Grabriella Gabriel,Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria wanawake (TAWLA),Lilian Mollel na Kaimu Katibu wa Tume ya marekebisho ya Sheria Nchini,Zainabu Chanzi wamesema huduma wanazozitoa katika wiki ya Sheria ni pamoja na msaada wa kisheria
No comments:
Post a Comment