HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 13, 2022

Dk.Mpango azindua Sera Mpya ya Taifa ya Mazingira ya 2021,atoa maagizo kwa viongozi wenye dhamana


Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akizindua Sera Mpya ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MAKAMU  wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango leo amezindua Sera Mpya  ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 na kumtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk. Selemani Jafo kuunda timu ambayo itakuwa chini ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Anthony Mtaka.

Timu hiyo ambayo itashirikiana na Halmashauri ya jiji la Dodoma, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS),na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),kuandaa mpango mkakati wa kukijanisha Mji na kumpa taarifa ya utekelezaji  ya kiuhalisia kila baada ya miezi mitatu.
 
Mbali na agizo hilo pia  Dk.Mpango ametoa maagizo mbalimbali likiwamo la Mawaziri wa Kilimo,Maliasili na Utalii maji,Mifugo na Uvuvi pamoja na Kamati ya Bunge ya uwekezaji na mazingira waende kufanya tathmini na kumpatia majibu  hatua walizochukua katika eneo la bwawa la Mwalimu Nyerere lililopo Rufiji.

Makamu wa Rais  ametoa maagizo hayo Leo Februari 12, 2022 Jijini Dodoma wakati akizinduzi Sera hiyo ambayo inaenda sambamba na Mpango wa Taifa wa Miaka mitano wa 2020/2021 hadi 2021/2026 na Mpango endelevu wa mwaka2030 na Mpango wa Miaka 15 ulioanza 2011/2012 mpaka 2025/206 ambapo ametoa maagizo hayo kufuatia kuwepo kwa uharibifu wa vyanzo vya Maji vilivyopo katika maeneo ya bwawa hilo.

Akizungumzia mkakati huo Dk.Mpango amesema kwenye utekelezaji huo pale itakapoonekana unalegalega wahusika wote wawajibike wenyewe kabla hajaingilia kati.

Ameongeza kuwa maelekezo hayo yanahusu kila Mkoa hivyo wahakikishe agizo hilo linafanyika na kwamba katika ziara zake zote atakazokuwa akizifanya agenda yake ni katika kuifanya ni kuhakikisha upendezeshaji wa usafi na  Mazingira ya kijani kwenye eneo husika hivyo amewata viongozi hao kujipanga.

Aidha amemtaka pia waziri Jafo kusimamia mchakato wa kuandaa mswada wa sheria utakayoakisi sera Mpya ambayo imezinduliwa.

"Nawapongeza wananchi wote wa Dodoma na wadau mbalimbali wa mazingira kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za uhifadhi wa mazingira tangu Februari 7, mwaka huu hadi kufikia leo na kwa namna ya kipekee napenda kumpongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ametuunga mkono kuja kupanda miti," amesema.

Ameongeza kwamba amefarijika kuona mwamko wa wakazi wa Dodoma kuifanya jiji hilo kuwa la kijani na kuwa sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo.

Makamu huyo wa Rais amesema kuwa taarifa alizozipata ni kwamba tangu  Februari 7 wamepanda miti maeneo ya Medeli,maeneo ya barabara ya Chimwaga hadi Iyumbu na kufanya usafi sehemu mbalimbali katika jiji hili pamoja na kutoa elimu.

"Mimi kama msimamizi mkuu wa mazingira mmenitia moyo sana hongereni sana wote mlioshiriki pamoja na vyombo vya  ulinzi na usalama wabunge na madiwani Mungu awabariki Sana," amesema Dk. Mpango.

Aidha amewapongeza viongozi katika mikoa mbalimbali ambao wanafanya jitihaha za kuweza kulinda na kuhifadhia mazingira pamoja kufanya usafi katika maeneo yao.

Awali  Dk.Jafo amesema kuwa Sera hiyo Itasaidia Tanzania kuwa sehemu salama katika suala zima la kutunza mazingira pamoja na kuongeza fursa katika suala la taka ambapo Sera imezingatia utekelezaji wa Mpango wa Taifa.

Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa kielelezo cha kutosha cha jinsi gani Taifa anavyolipeleka mbele ambapo kazi yao ni kuyatekeleza maagizo anayoyatoa.

Amesema kuwa awali kulikuwa na sera ya mwaka 1997 ambayo ilipata mafanikio makubwa katika kutekeleza masuala mbalimbali ya kimazingira iliyozalisha sheria ya namba 20 ya mwaka 2004 na kuzalisha kanuni zake.

"Sasa kuona kuna uhitaji kwamba kulikuwa na mataifa na matamko mbalimbali ya kimataifa ya mabadiliko ya matakwa ya kimazingira yalisababisha kuanza mchakato wa sera mpya ya mazingira, chini ya utawala wako Makamu wa Rais tumeweza kupata Sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 2021 ambayo unazindua leo," amesema.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji na Mazingira ,David Kihenzile amesema mefurahia kubadilishwa kwa Sera ya Mazingira ambayo imedumu muda mrefu huku akitoa rai kwa Serikali kufanya mchakato kwenda kwenye Sheria na kanuni.

Uzinduzi huo umeenda sambamba na kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira ambayo yalianza rasmi February 7 Mwaka huu ambayo iliambatana na upandaji miti pamoja na usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya Dodoma na yamehitimishwa na kaulimbiu isemayo

No comments:

Post a Comment

Pages