HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2022

Kunenge apania makubwa sekta ya viwanda

 


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa baraza la biashara la Mkoa huo.

 

Na Victor Masangu, Pwani


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge l amefungua  mkutano wa baraza la biashara la Mkoa kwa ajili ya kujadili kero na changamoto zinazowakabili wawekezaji pamoja na wafanyabiashara lengo ikiwa ni kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ambayo itasaidia kuongeza kasi katika kukuza uchumi.

Katika mkutano huo ambao umehudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wakuu wa wilaya,wakurugenzi,wawekezaji pamoja na wafanyabiashara una lengo la kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia sekta ya biashara.

Mkuu huyo amesema kuwa kwa sasa lengo kubwa la Mkoa wa Pwani ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega na wawekezaji wote pamoja na wafanyabiashara kwa kuwawekea mazingira wezeshi ambayo yatawasaidia katika kutimiza malengo yao.

 Aidha aliongeza kuwa katika kufikia malengo ambayo wamejiwekea watahakikisha wanaboresha zaidi huduma ya nishati ya umeme pamoja na miundombinu ya barabara ili kuwapa fursa wawekezaji hao kupata huduma stahiki.

 "Katika kikao hiki kitu kikubwa ninachowaomba tujadili mambo ya msingi ambayo yataweza kuleta athari ambazo ni chanya katika suala zima la kufanya biashara zetu ambazo zitakuwa na tija zaidi katika kukuza pato la Taifa,"alisema Kunenge.

 Pia alifafanua kwamba ana Imani kubwa kutoka na Mkoa wa Pwani unaongoza kwa viwanda nchi nzima wawekezaji na wafanyabiashara wakiwekewa mifumo mizuri ya kuwasaidia kwa kushirikiana na taasisi wezeshi kutaweza kuleta sura mpya na mabadiliko ya kimaendeleo kwa Mkoa wa Pwani.

  "Ukiangalia kwa sasa tuna jumla ya idadi ya viwanda vipatavyo 1453 ambayo Kati ya hivyo Kuna vya kati,vidogo pamoja na vikubwa na uzuri vyote hivi tumeshavifanyia uhakiki kwa hiyo tunazidi kupiga hatua,"alisisitiza Kunenge.


 Pia alimpongeza Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani kwa vitendo katika sekta mbali mbali ikiwemo kutaja vipaumbele vyake nane ambavyo viongozi na watendaji wanapaswa kuvitekeleza katika maeneo yao. 

Kunenge pia aliongeza kuwa vipaumbele vyote nane ambavyo vimetajwa na Rais Mama Samia Suluhu vyote vipo katika maeneo ya Mkoa wa Pwani ikiwemo suala la kuwa na uchumi wa bluu ikiwemo ufugaji,kilimo uvuvi wa baharini pamoja na kutunza mazingira.

 Kwa Upande wake Katibu  Tawala wa Mkoa wa Pwani Mwanasha Tumbo alisema kwamba mkutano huo wa baraza la biashara litaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa upande wa wawekezaji pamoja na wafanyabiashara wadogo pamoja na wakubwa. 

Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamempongeza Rais wa awamu ya sita kwa juhudi zake za kuhakikisha anaweka mipango mizuri ya kuwasaidia wawekezaji ili waweze kuwekeza katika Mkoa wa Pwani na kwamba anatekeleza ilani ya chama kwa vitendo. 

No comments:

Post a Comment

Pages