Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
MAKAMU
wa Rais Dokta Philip Mpango anatarajiwa kuzindua Sera mpya ya Taifa ya
Mazingira ya Mwaka 2021 iliyojumuisha mambo sita yaliyokuwepo katika
Sera ya Mwaka 1997 ikiwemo udhibiti wa taka za kielectroniki.
Mambo
mengine ni Usimamizi na Matumizi ya kemikali,mabadiliko ya
tabianchi,udhibiti wa viumbe vamizi,Usimamizi wa Matumizi salama ya
bioteknolojia ya kisasa na udhibiti wa Uchaguzi katika shughuli za
utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Jijini Dodoma Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira
Marry Maganga amesema Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira itafanyika Februari 12,Mwaka huu.
Amesema
Sera mpya ya Mazingira imeongeza wigo wa masuala na changamoto za
Mazingira zinazopaswa kufanyiwa kazi katika kipindi husika Ili kuleta
maendeleo endevu na pia imezingatia changamoto mpya za kimazingira
zinazoendelea kujitokeza kutokana na mabadiliko ya mifumo ya
kiuchumi,kijamii na kimazingira yanayoendelea duniani.
"Dhumuni
ya kuwepo kwa shughuli hizo ni pamoja na kurejesha hali ya asili ya
Mazingira iliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu kwa kuwa na
zoezi la upandaji Miti Ili kuwa na Mazingira safi"Alisema
Aidha
amesema kabla ya Uzinduzi wa Sera huo,kutakuwa na wiki ya Mazingira
itakayoanza Februari 7 hadi 12 ambapo shughuli mbalimbali za hifadhi ya
Mazingira zitafanyika ikiwa ni sehemu ya masuala ya msingi
yanayoelekezwa katika Sera mpya.
Ametaja
shughuli hizo kuwa ni pamoja na upandaji Miti katika eneo la
Medeli,Iyumbu,Isern,maeneo ya barabara inayoanzia Chimwaga ,Chuo Kikuu
Cha Dodoma kuelekea barabara ya Dodoma Dar es Salaam,kutoa Elimu kuhusu
utenganishi wa taka na kufanya usafi katika soko la Chang'ombe na utoaji
wa Elimu ya Mazingira wa wananchi na wadau kupitia vyombo vya habari.
Amesema
kutakuwa na shughuli za usafi wa Mazingira zinazolenga kuboresha afya
ya jamiii na Elimu na Elimu ya utenganishaji taka kwa ajili ya
udhibiti wa taka ngumu wa kumwezesha urejelezaji wa taka kwenye bidhaa
na huduma mbalimbali.
No comments:
Post a Comment