Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Sulemani Jafo amesema kuwa Athari za uharibifu wa mazingira zimesababisha ukame na kupelekea nchi kuingia katika mgao wa umeme.
Amesema ukame huo umepelekea athari ya kiuchumi kwani wakulima walishindwa kuzalisha mazao kipato kikashuka wafugaji walipoteza mifugo kipato kikashuka pia maji yalishindwa kutiririka kilimo cha umwagiliaji kikashindikana na hata mabwawa yanayotumia maji kuzalisha umeme ilichindikana na kupeleka umeme kuwa mdogo.
Katika uzinduzi wa Bodi ya baraza la Uhifadhi wa Mazingira Nchini (NEMC) Waziri huyo amesema kuwa kutokana na hayo ajenda ya Mazingira ni Muhimu kwa mstakabali wa taifa lakini pia ameeleza ajenda hiyo ni ya kidunia.
"Nikuweli usiopingika bila kusimamia vizuri suala la Mazingira dunia itakuwa katika changamoto kubwa na ndio maana dunia yote kwa umoja inajadili suala zima la mazingira na ndio maana hata katika mikutano ya Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa dira ya taifa katika upande wa Mazingira," amesema Waziri Jafo.
Katika miezi michache kabla ya mvua kunyesha maji yalikuwa machache tumeona uhaba wa maji ulikuwa mkubwa kupita kiasi ni kwa sababu vyanzo vya maji vingi vilikuwa vikitiririsha maji chini ya uwezo na kupelekea mgao wa maji kwa baadhi ya mikoa ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam huku wanyama wakifa yote ni mbadailiko ya tabia nchi .
"Leo hii tunapo zindua bodi hii ambalo jukumu lake kubwa ni kwenda kusimamia masuala mazima ya Mazingira NEMC tunaimani kuwa mtakwenda kufanya vizuri kama matarajio yetu muende mkafanye kazi kwa ubora zaidi ili nchi yetu iweze kusonga mbele," amesema
Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga amempongeza Mwenyekiti Prof. Esnati Chaggu na wajumbe wa Bodi hiyo kwa kuchaguliwa kuongoza Taasisi hiyo yenye jukumu kubwa la kusimamia masuala ya mazingira Nchini.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wa Bodi, Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Profesa Mhandisi Chaggu amesema wana dhamana kubwa katika kuhakikisha agenda ya mazingira inapewa msukumo wa dhati kwa kuwa ni mjadala wa dunia kwa sasa.
February 08, 2022
Home
Unlabelled
UHARIBIFU WA MAZINGIRA NA ATHARI ZA KIUCHUMI
UHARIBIFU WA MAZINGIRA NA ATHARI ZA KIUCHUMI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment