HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 03, 2022

Marie Stopes waanza kampeni saratani ya mlango wa kizazi


 

Na Irene Mark
 
KUELEKEA siku ya kilele cha Saratani Duniani inayoadhimishwa kila Februari 4 ya mwaka, Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST) limeanza kampeni ya siku 14 kuelimisha kuhusu saratani hasa ya mlango wa kizazi.
 
Akizungumza na Habari Mseto Blog, Meneja wa Masoko Bi, Esther Shedafa anasema shirika hilo kupitia Hospitali ya Mwenge iliopo Mwenge Dar es Salaam na vituo vyake vingine vilipo maeneo mbalimbali hapa Tanzania watatoa elimu  ya saratani ya mlango wa kizazi, huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti, upimaji wa shinikizo la damu, upimaji wa uzito na kupatiwa elimu ya njia za afya ya uzazi na huduma ya njia za afya ya uzazi kwa wahitaji.

“Huduma hizi zote zitatolewa kwa sh. 5,000 ili kuhakikisha tunawafikia watanzania wengi kupata huduma hiyo ya saratani, afya ya uzazi na afya kwa ujumla,” amesema Shedafa.

Kwa mujibu wa meneja masoko huyo, huduma hizo zitaanza kutolewa kwenye vituo vyote vya Marie Stopes kuanzia Februari 4 mpaka Februari 14.
 
“...Leo Februari 3, 2022 tunatangaza kuanza rasmi kwa kampeni hiyo tukiwashauri watanzania kufika kwa wingi kwenye hospitali na vituo vyetu vya afya vilivyo karibu ili kupata huduma hizo,” anasema Shedafa.
 
Anasema ili kufanikisha kampeni hiyo amewakaribisha pia wanahabari kusaidia kuitangaza ili watanzania wasikie na kuitumia fursa hiyo vizuri.

Huduma hizo zinatolewa kwenye Hospitali ya Marie Stopes Mwenge jijini Dar es Salaam.

Vituo vingine vya MST vinavyotoa huduma hizo ni Kimara, Mwanza, Arusha, Kahama, Musoma, Iringa, Makambako, Mbeya na Zanzibar.
 

No comments:

Post a Comment

Pages