Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,amesema atawachukulia hatua baadhi ya Maafisa mabonde ya Maji ambao watabainika kutumia vibaya fedha za utekelezaji wa miradi ya Maji.
Waziri Aweso ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiliaji Saini baina ya Wizara ya Maji kupitia idara ya rasilimali za maji hati ya makubaliano na Wakala wa Maji vijijini (RUWASA)kuhusu utaratibu wa utekelezaji wa miradi ya mabwawa ya maji kwenye maeneo yanayoratibiwa na RUWASA .
Katika hatua nyingine Waziri Aweso amesema kuna haja ya Wizara Mtambuka kuungana kwa pamoja na kujenga bwawa katika kurahisisha uvunaji wa maji ya mvua .
Kwa Upande wao Mkurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijini RUWASA Mhandi Clement kivegalo pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya rasilimali za maji George Lugomelo wakaeleza mikakati wanayotekeleza katika kuwahudumia wananchi.
Pia Waziri Aweso amesema serikali inafanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji ya kuhakikisha kuwa huduma ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini inaboreshwa huku akitaka maadhimisho ya wiki ya Maji ambayo hufanyika Mwezi Machi kuanzia tarehe15 hadi 22 kutumika kuzindua miradi mbalimbali pamoja na kujitathmini katika utendaji kazi wao.
No comments:
Post a Comment