Meneja
wa NEMC Kanda ya Kati Dk. Franklin Rwezimula akiwa katika zoezi la
upandaji mti wakati wa kutekeleza kampeni ya usafi na upandaji miti kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na wananchi wa
Kata ya Chang'ombe leo Tarehe 5/02/2022. (Picha na NEMC).
Mkurugenzi
wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru akiwa katika zoezi la upandaji mti
wakati wa kutekeleza kampeni ya usafi na kupanda miti kwa kushirikiana
na wananchi pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira -NEMC katika Kata ya Chang'ombe jijini Dodoma leo Tarehe
5/02/2022.
Baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC wakifanya usafi wa mazingira pamoja na wananchi kwa kushirikiana na maafisa wa jiji la Dodoma wakati wa zoezi la usafi na upandaji miti lililofanyika Kata ya Chang'ombe jijini Dodoma leo tarehe 5/02/2022.
Mkurugenzi
wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru akishirikiana na wananchi waliojitokeza katika zoezi la usafi na upandaji miti lililofanyika Kata ya Chang'ombe jijini Dodoma leo tarehe 5/02/2022.
No comments:
Post a Comment