JUMLA
ya wateja 600 wa Benki ya NMB wamejishindia shilingi milioni 60 katika
droo ya kila wiki ya 'NMB Mastabata Kivyakovyako ililiyofanyika jijini
Dar es Salaam.
MastaBata ni
kampeni inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikihamasisha Watanzania kuendana
na kasi ya dunia ya dijitali, ya matumizi yasiyohusisha pesa taslimu,
huku benki hiyo ikitenga zaidi ya Sh. Mil. 200 kama motisha kwa wateja
wanaotumia zaidi kadi zao za MasterCard, Masterpass QR, Vituo vya Mauzo
(PoS).
Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo, Ofisa
Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Lightness Zablon, amesema kuwa
Kampeni ya NMB Mastabata Kivyakovyao inawahimiza wataje wanaotumia
Mastercard katika malipo ya mtandaoni kwa kutumia mashine za Masterpass QR, Vituo vya Mauzo
(PoS).
"Ulimwengu umebadilika na matumizi ya pesa taslimu yana gharama kubwa, zikiwamo za upotevu, wizi na uporaji na kwamba Watanzania wanapaswa kuendana na kasi ya mabadiliko hayo kwa kujikita katika matumizi kwa njia ya kadi." Alisema Lightness.
Kufikia sasa, kampeni hiyo iliyoanza mwishoni mwa Desemba
mwaka jana, imeshatoa zawadi za pesa taslimu kiasi cha Sh. Mil. 85 kwa
wateja 625, ambazo ni kati ya zaidi ya Sh. Mil. 200, zitakazotolewa kwa
wateja 1,080 katika kipindi cha wiki 10 za kampeni hiyo, inayofanyika
kwa msimu wa tatu. Fainali ya NMB MastaBata itafanyika Machi mwaka huu.
Ofisa Huduma kwa Wateja Benki ya NMB, Lightness Zablon, akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya sita ya Kampeni ya ‘NMB Mastabata Kivyako Vyako’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Hudama kwa Wateja, Susan Manga na kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzana (GBT), Elibariki Sengasenga. (Na Mpigapicha Wetu).
Ofisa Huduma kwa Wateja Benki ya NMB, Lightness Zablon, akibonyeza kitufe cha kompyuta kumtafuta mmoja kati ya washindi 100 wa droo ya sita ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata - Kivyako Vyako’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja, Susan Manga na kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo tya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga.
No comments:
Post a Comment