HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 11, 2022

CRDB, ATCL watoa zawadi kwa washindi wa Promosheniya Siku ya Wapendanao

 
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Masoko Benki ya CRDB, Joe Bendera (katikati), akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa Promosheni Maalum katika kuelekea msimu wa wapendanao, yenye lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya manunuzi kwa njia ya kadi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, AIR Tanzania, Edward Nkwabi na kulia ni Kaimu Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi CRDB, Erica Mwaipopo. 
 
Bendera amesema jumla ya washindi 10 wamepatikana baada ya kutuma video zao  zikiwa na maelezo ya watu gani watatu ambao wanawapenda au wanataka kwenda nao katika tamasha la Sauti za Busara ambapo Benki ya CRDB kwa kushirikiana na ATCL ambayo itagharamia safari yao katika tamasha hilo.
 
Kampeni hii ilitoa fursa kwa wateja wa benki ya CRDB kurekodi video fupi ya sekunde 60 na kutoa maelezo ya watu gani watatu ambao anawapenda au anataka kwenda nao katika tamasha la Sauti za Busara ambapo Benki ya CRDB kwa kushirikiana na ATCL imetoa tiketi za ndege kwa washindi hao kwenda kushuhudia tamasha hilo linalofanyika Mji Mkongwe Zanzibar huku Benki ya CRDB ikigharamia hoteli watakazofikia pamoja na chakula.   
 
Benki ya CRDB imekuwa mshirika na mdhamini Mkuu wa Tamasha la Busara linalofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar.
Washindi wakiwa na furaha.
Heavenlight Paul ambaye ni mmoja wa washindi akizungumza baada ya kupokea tiketi yake.
Magwila Mwasyoke ambaye ni mfanyakazi wa benki ya CRDB akiwa ni miongoni mwa washindi wa shindano hilo.
 
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages