Afisa Mkuu
wa Wateja Binafsi na Biashara benki ya NMB, Filbert Mponzi, akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, moja kati ya kompyuta
mpakato 5 zilizotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya Shirikisho la Umoja wa
Machinga Tanzania (SHIUMA). Kushoto ni Katibu wa Machinga Kariakoo, Thabit
Maloka na kulia ni Meneja Mahusiano Biashara za Serikali Benki ya NMB, Mkunde
Joseph. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Hassan Zungu
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, ameishukuru
Benki ya NMB kwa kulikumbuka kundi la wafanyabishara ndogo ndogo nchini
maarufu Wamachinga na kuwasaidia kukua.
Benki ya NMB ilimkabidhi Naibu Spika laptop 5 zenye thamani ya Tsh. Milioni 7.5 kusaidia upatikanaji wa database wa kundi hilo.
Baada
ya kupokea vifaa hivyo, Mh. Mussa Hassan Zungu alivikabidhi kwa
viongozi wa SHIUMA, tawi la Ilala kwa ajili ya matumizi ya kiofisi
ikiwemo kuweka Kanzi Data(database), ili iwe rahisi kutambulika na kujua
shughuli wanazofanya popote walipo nchini.
Zungu
ameisifu NMB kuwa ni benki ya kipekee iliyoonyesha kwa vitendo kujali
maisha ya wafanyabiashara wadogo, kwa kuwasaidia mitaji na kuangalia
ukuaji wao.
Afisa Mkuu wa
Wateja Binafsi NMB, Filbert Mponzi alisema vifaa hivyo ni mwendelezo wa
makubaliano waliyoingia kati yao na SHIUMA, lengo ni kutengeneza Kanzi
Data itakayowasaidia kujulikana kirahisi na kufikika.
Pia, angependea kuona Wamachinga wamesajiliwa, wawe rahisi kufikika.
Alibainisha
kuwa pamoja na makabidhiano ya vifaa hivyo, NMB imeendelea kushirikiana
na kundi hilo la wafanyabiashara wadogo tangu mwaka 2000. Kwa wastani,
benki ya NMB hutoa mikopo ya thamani ya Sh Bil 50 kila mwezi kwa kundi
hilo la wafanyabishara wadogo wakiwemo Wamachinga.
Kwa
upande wake Katibu wa Wamachinga Kariakoo, Thabit Maloka
aliyemwakilisha Mwenyekiti wa SHIUMA Taifa, alisema wamepata faraja
kubwa kwa msaada huo kutoka NMB, wanaamini hayo ni matunda ya Serikali
ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na ahadi
aliyowapa kuwashika mkono.
Alibainisha
kuwa wanaamini huo ni mwanzo tu, kwani wanajua mazuri yanakuja. Ambapo
aliuomba uongozi wa NMB kufikiria kuongeza msaada zaidi ikiwemo kufanya
ukarabati wa majeng ya ofisi zao za Ilala jijini Dar es Salaam pamoja na
kuwapa mafunzo ya ujasiriamali.
Kompyuta hizo tano
zinakwenda kujenga mifumo ya mawasiliano, ufuatiliaji na tathmini
katika shughuli za Wamachinga pamojaa na kuwasaidia Wamachinga kuwa na
mfumo mzuri wa kufanya biashara zao.
No comments:
Post a Comment