HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 22, 2022

Serikali yakabidhi rasmi kiwanda cha chai Mponde kwa WCF, PSSSF

*Uzalishaji kuanza haraka, ajira kurejea baada ya miaka 10


Msajili wa Hazinaa, Mgonya Benedicto akisaini nyaraka wakati wa makabidhiano ya Kiwanda cha Chai Mponde yaliyofanyika jana jijini Dodoma kati ya Serikali na Kampuni ya Mponde Holding inayomilikiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya WCF na PSSSF ambazo kila moja ina hisa asilimia 42 wakati Serikali inamiliki asilimia 16 zinazosimamiwa na Msajili wa Hazina. Aliyesimama ni Mwanasheria katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Asimuna Kipingu. (Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina).
 Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto akimshuhudia Mjumbe wa Bodi wa Kampuni ya Mponde Holding, Paul Kijazi akisaini nyaraka za makabidhiano ya Kiwanda cha Chai Mponde kilichokuwa kimefungwa kwa takribani miaka 10, lakini sasa kiko mbioni kuanza uzalishaji baadhi ya kuchukuliwa na kampuni hiyo inayomilikiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya WCF na PSSSF kwa asilimia 42 kila moja huku Serikali ikiwa na asilimia 16 zinazosimamiwa na Msajili wa Hazina. Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dodoma. Wengine wanaoshuhudia pichani ni Mwanasheria katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Asimuna Kipingu (aliyesimama) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dk John Mduma.
 Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (kushoto) akikabidhi nyaraka za umiliki wa Kiwanda cha Chai Mponde kwa Mjumbe was Bodi ya Kampuni ya Mponde Holding, Paul Kijazi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya kiwanda, mali na nyaraka. Kiwanda hicho ambacho kilifungwa kwa tarikabni miaka kumi, kwa sasa kinamilikiwa na Kampuni ya Mponde Holding, mali ya WCF na PSSSF zenye asilimia 42 kila moja na Serikali ambayo ina hisa 16 zinazosimamiwa na Msajili wa Hazina. (Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina).
 Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (katikati) akisoma maelezo ya awali kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya Kiwanda cha Chai Mponde jana jijini Dodoma. Kushoto kwa Msajili wa Hazina ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wanyakazi (WCF), Dk John Mduma (kushoto) na Fortunatus Magambo, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Wengine kulia kwa Msajili wa Hazina ni Mohamed Nyasama, Mkurugenzi wa Ubinafsishaji katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hoseah Kashimba na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Mponde Holding inayomilikiwa na WCF na PSSSF, Paul Kijazi. Mbali ya WCF na PSSSF zenye asilimia 42 kila moja, Serikali pia ni mmiliki katika kiwanda hicho, ikiwa na asilimia 16 zinazosimamiwa na Msajili wa Hazina.

 

Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Ubinafsishaji katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mohamed Nyasama na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Hoseah Kashimba muda mfupi kabla ya makabidhiano ya Kiwanda cha Chai Mponde jana jijini Dodoma. Kiwanda hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Mponde Holding, mali ya WCF na PSSSF zenye asilimia 42 kila moja na Serikali ambayo ina hisa 16 zinazosimamiwa na Msajili wa Hazina.

Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wanyakazi (WCF), Dk John Mduma (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Hoseah Kashimba muda mfupi kabla ya makabidhiano ya Kiwanda cha Chai Mponde kilichokuwa kimefungwa kwa takribani miaka 10, lakini sasa kiko mbioni kuanza uzalishaji baadhi ya kuchukuliwa na WCF na PSSSF kwa hisa asilimia 42 kila moja huku Serikali ikiwa na asilimia 16 zinazosimamiwa na Msajili wa Hazina. Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dodoma.
 
 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 

 

BAADA ya kushindwa kufanya kazi kwa takribani miaka kumi kutokana na sababu mbalimbali, hatimaye Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imekabidhi Kiwanda cha Chai Mponde kwa Kampuni ya Mponde Holding inayomilikiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya WCF na PSSSF iliyoomba kufanya uwekezaji na kuendeleza kiwanda hicho.

 

Mifuko hiyo inamiliki hisa asilimia 84, kila mmoja ukiwa na asilimia 42 wakati asilimia nyingine 16 zinamilikiwa na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina.

 

Makabidhiano ya kiwanda ikiwa ni pamoja na hati, mali na nyaraka mbalimbali yalifanyika jana jijini Dodoma kati ya Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto kwa niaba ya Serikali na mwakilishi wa Mponde Holding Company ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni hiyo, Paul Kijazi. Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF CPA Hoseah Kashimba na mwenzake wa WCF, Dk John Mduma PSSSF, walikuwa miongoni mwa walioshuhudia makabidhiano hayo.

 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mgonya alisema Serikali imeona vyema mali na nyaraka zikakabidhiwa kwa uongozi wa Kampuni ili kuruhusu baadhi ya mambo muhimu yaliyohitaji nyaraka hizo kuendelea ili hatimaye shughuli za uzalishaji ziweze kuanza mara moja.

 

“Ofisi yangu inatoa shukrani za dhati kwa Bodi ya Kampuni ya Mponde Holding pamoja na Uongozi wa Mifuko ya PSSSF na WCF kwa ushirikiano na jitihada kubwa mnazofanya katika kuhakikisha kiwanda cha Mponde kinarejea katika kuzalisha na hatimaye wananchi wapate ajira tena baada ya muda mrefu kupita.

 

“Ofisi yangu itaendelea kutoa ushirikiano stahiki kila itakapohitajika kwa lengo la kuhakikisha madhumuni yaliyokusudiwa katika kufufua kiwanda cha Mponde yanafikiwa,” alisema Msajili wa Hazina.

 

Kiwanda hicho kilifungwa tangu mwaka 2013, baada ya mwekezaji katika Kiwanda cha Chai cha Mponde – Umoja wa Wakulima wa Chai Usambara (UTEGA – Usambara Tea Glowers Association) kukiuka masharti ya ubinafsishaji na Serikali kujiridhisha pasipo shaka kwamba, mwekezaji huyo hakuwa na mpango wala nia ya dhati ya kukiendeleza kiwanda hicho.

 

Kutokana na hali hiyo, Serikali iliamua kukirejesha kiwanda kama Mkataba unavyoelekeza. Urejeshaji wa kiwanda hicho ulifanyika Januari, 2016.

 

Mbali na Hati na nyaraka, Msajili wa Hazina pia amekabidhi magari matatu mali ya kiwanda hicho.

 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kiwanda, mali na nyaraka hizo, Mjumbe wa Bodi ya Mponde Holding, Paul Kijazi aliishukuru Serikali kwa uamuzi wa kuwakabidhi kiwanda huku akiahidi kufanya kila linalowezekana kufikia malengo katika uwekezaji wao unaotarajiwa kuleta manufaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ajira, kuendeleza zao la chai na pia kuchangia katika ukuaji wa pato la taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages