HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 15, 2022

Wanawake Burunge WMA wapewa ruzuku kukopeshana


Mwandishi Wetu, Babati


WANAWAKE wakiwepo wa jamii ya Kibarbeig katika eneo la Hifadhi ya Jamii ya  Wanyamapori (WMA), ya Burunge wamepewa  ruzuku ya Sh. milioni 16 na Taasisi ya Chemchem Association ili wakopeshane.

Meneja wa Chemchem Association  ambayo ni taasisi iliyopo chini ya mwekezaji wa shughuli za Utalii ya Chemchem, Walter Pallangyo alisema lengo la kutoa ruzuku hiyo, ni kuongeza uwezo wa vikundi kukopeshana na kutambua mchango wa wanawake katika uhifadhi.

Pallangyo alikabidhi milioni saba, kwa vikundi saba, ikiwa ni awamu ya pili baada ya kupewa Sh. million tisa.

Alisema Chemchem kama wawekezaji katika eneo hilo, ambao wanafanya utalii wa picha na hoteli za kitalii, wanataka wanawake katika eneo hilo, kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa uhifadhi, kupiga vita ujangili na kunufaika na utalii.

Walter alisema kutokana na faida za uhifadhi chemchem katika eneo hilo tayari imetoa bus ya usafiri wa wanafunzi, imejenga madarasa, imekarabati nyumba za walimu na vyoo, imejenga vituo vya afya na kununua madawati kwa shule zilizopo katika eneo hilo la hifadhi ya jamii.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Vilima vitatu, wilayani Babati, Seleman Juma alisema kutolewa na fedha hiyo faida ya kutunza mazingira, kupiga vita ujangili .

Aliwataka wanawake hao kutumia fedha hizo kama ilivyokusudiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa vikundi vilivyonufaika, Flora Godson alishukuru Chemchem kwa msaada huo na kueleza watatumia fedha hizo kama ilivyokususudiwa kwa kukopeshana na kuzalisha faida.

Alisema fedha hizo zitaongeza mikopo yao na hivyo kupanua biashara zao.


No comments:

Post a Comment

Pages