Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio uliofanyika leo Mei 18,2022 kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza Halmashauri na mikoa yote hapa nchini,kuhakikisha inatoa elimu kwa wananchi kuhusu chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa miaka sifuri hadi mitano ili kuwaepusha na ugonjwa huo ambao hauba tiba.
Pia amesema kuwa serikali kupitia wizara ya afya inatarajia kutoa chanjo katika mikoa mikoa 21 ya Tanzania ambapo kwa siku nne za utoaji chanjo hiyo Serikali imelenga kuwafikia na kuchanja watoto 10,295,316
Waziri Ummy ameyasema hayo Mei 18,2022 wakati akizindua kampeni ya pili ya chanjo ya polio Mkoani Dodoma kwa watoto wenye umri kuanzia sifuri hadi miaka mitano amessma kuwa Halmashauri zote lazima zielekeze fedha kwenye utoaji wa chanjo kwa watoto kwani ndiyo kinga yao dhidi yaa ugonjwa huo.
Amesema kuwa asilimia 5 hadi 10 ya watu huonesha dalili hafifu za homa, maumivu ya kichwa, kutapika, kuharisha, mishipa ya shingo kukaza na maumivu katika miguu na mikono huku athari zake zikielezwa kuwa ni mgonjwa kupata ulemavu wa kudumu.
"Takriban asilimia 90 hadi 95 ya wanaoambukizwa ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote, Ugonjwa huu hauna tiba lakini kinga ipo,nawasihi wazazi na walezi muwapeleka watoto kupata chanjo," amesema waziri Ummy.
Waziri Ummy ameongeza kuwa baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo Viongozi wa Halmashauri waatekeleze majukumu ya utoaji chanjo katika Zahati,vituo vya Afya,kwa njia ya Tembezi,Mkoba pamoja na kupita nyumba kwa nyuumba.
Aidha amewataka viongozi katika halmshauri mbalimbali wakatoe elimu kwa jamii ili kuepusha uvumi uliopo miongoni mwa jamii kwamba chanjo hiyo ina madhaa kwa watoto.
“Katika hili,Mkurugenzi wa Afya TAMISEMI naomba mkasimamie,hakikisheni wenyeviti wa vijiji pamoja na viongozi wa serikali za mitaa wanatoa elimu sahihi kuhusu ya chanjo hii kwa wananch.”alisema Ummy
Aidha Ummy alisema,baada ya uzinduzi huo wanatarajia kutoa chanjo katika mikoa mikoa 21 ya Tanzania ambapo kwa siku nne za utoaji chanjo hiyo Serikali imelenga kuwafikia na kuchanja watoto 10,295,316
“Zoezi la utoaji chanjo hiyo litakuwa la siku nne kwa nchi nzima na huduma zitatolewa katika vituo vya kutoa huduma za afya,ikiwemo Zahati,Vituo vya Afya,Hospitali,,lakini kutokana na kufahamu wazazi wanashughuli zao,hivyo zoezi hilo litafanyika kwa njia tembezi na Mkoba ikiwemo kuwafuata maeneo watoto walipo ili kuwakinga watoto,”
Vile vile kwa upande wa Zanzibar wanalenga kuchanja watoto takribani 281,489 ambapo jumla Bara na Visiwani wanatarajia kuchanja watoto 10,500,000.
Ummy amewataka wazazi na walezi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ambao kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani ugonjwa huo upo Msumbiji huku akisema ni vyema watoto wapelekwe kupata chanjo ili kuwakinga dhidi ya polio.
Amewataka wataalamu wa afya kuimarisha huduma za utoaji wa chanjo kwa kipindi chote cha kampeni na baada ya kampeni na kuongeza serikali haijasimamisha utoaji wa chanjo nyingine kwa sababu watoto bado wanazaliwa
Mbali hilo Waziri Ummy amwaagiza viongozi katika halmashauri na mikoa kuhakikisha fedha zilizotolewa kwa ajili ya kampeni ya ugonjwa wa Polio,zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na siyo vinginevyo.
No comments:
Post a Comment