Diwani wa Kata ya Nianjema iliyopo katika Halmashauri
ya Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Abdul Pyalla wa Kati kati aliyevaa kofia
akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Magomeni na Nianjema wakiwa katika mkutano huo kumsikiliza diwani wa kata ya Nianjema.
Na Victor Masangu, Bagamoyo
Diwani
wa Kata ya Nianjema katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Samia
Suluhu Hassan katika kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi ameamua
kufanya ziara ya kikazi kwa kutembelea mtaa kwa mtaa lengo ikiwa ni
kusililiza kero na changamoto zinazowakabili wananchi.
Akizungumza
na baadhi ya wananchi wa mitaa ya Magomeni A pamoja mtaa wa Nianjema B
Diwani huyo Mhe.Abdul Pyalla alisema kwamba ameamua kuwatembelea
wananchi ili kuweza kusililiza kero zao mbali mbali na kuweza
kuzitatutia ufumbuzi.
Alifafanua
kuwa katika ziara hiyo amejipanga vilivyo kutokana na kuambatana na
wataalamu mbali mbali kutoka taasisi za serikali pamoja na mashirika ya
umma nia na madhumuni ni kupata majibu ya kina kutoka kwa wataalamu
husika.
"Ziara yangu hii
lengo lake kubwa ni kutembelea mitaa mbali mbali ambayo ipo katika kata
yangu ya Nianjema na dhumuni lake kubwa ni kusililiza kero na changamoto
mbali mbali zinazowakabili wananchi wangu katika sekta tofauti,"alisema
Diwani huyo.
Aidha
aliongeza kuwa lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba anaweka mipango
madhubuti kwa kushirikiana na viongozi wenzake pamoja na taasisi za
kiserikali kwa kuwaletea huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo upatikani
wa umeme,maji,afya elimu pamoja na mahitaji mengine.
"Nashukuru pia katika mkutano huu tumeshirikiana kwa ukaribu na taasisi tofauti Kama vile Tanesco,Dawasa,Tarura,TFS, pamoja
na wenzetu wa benki ya NMB ambao wameweza kutoa fursa ya utoaji wa
elimu mbali mbali na umuhimu wa kujiunga na bima kupitia benki
hiyo,"alifafanua Diwani huyo.
Katika
hatua nyingine aliahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na taasisi
zote za kiserikali pamoja na mashirika ya umma kwa lengo la kuweza
kutatua changamoto za wananchi na kuweka mipango ya pamoja katika
kuwaletea maendeleo yenye tija kwa wote.
No comments:
Post a Comment