Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu 396 kwa
tuhuma mbalimbali za kiuhalifu ikiwemo unyang'anyi wa kutumia silaha,
kupanga njama za kufanya uhalifu, wizi wa magari, pikipiki, makosa ya
jinai pamoja na dawa za kulevya.
Akizungumza
na wanahabari jijini humo Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema
katika oparesheni iliyoanza Mei 15 hadi Juni 16 mwaka huu walifanikiwa
kuwakamata watu wanne kwa kupanga za uhalifu wa unyang'anyi wa kutumia
nondo na mapanga.
" Tumewakata watuhumiwa kwa
makosa mbalimbali wakituhumiwa makosa ya kiuhalifu yakiwemo ya wizi wa
magari, dawa za kulevya, kupanga njama hatua za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao," amesema Kamanda Muliro.
Amebainisha
kuwa katika oparesheni hiyo Mtuhumiwa Mohamed Bakari na wenzake 12
wanashikiliwa kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha ikiwemo visu
na mapanga na kwamba walijeruhi na kupora simu pamoja na laptop.
Kamnda
Muliro amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na ulinzi shirikishi
wamefanikiwa kuzipata silaha mbili aina ya pistol zikiwa na risasi 43
ambapo ya pili ilikamatwa Mbagala ikifichwa kwenye matuta.
Amesisitiza
kuwa katika tukio la uvunjaji wanamshikilia Omari Wilani (42) mkazi wa
Buza na wenzake ambapo walikutwa na TV 8 na Sh 300,000 ikiwa sehemu ya
mauzo ya vitu hivyo.
Ameongeza kuwa watuhumiwa
wa wizi wa magari 15 wamekamatwa na vipuri vya mgari kukutwa huku
akikbainisha magari mawili yamepatikana aina ya Suzuki Carry Namba
T-617 DRU na Toyota Wish 106 DNV.
Pia amesema
watuhumiwa hao wamekutwa na vipuri vya magari yaliyoiba, site miller
38, vibao vya namba za magari 47, taa za nyuma 14, injini 3 za
pikipiki,Rimu za matairi, mlango wa Prado na kadi za usajili wa magari.
Amefafanua
kuwa jeshi hilo linamshikilia Thabit Idd na wenzake 24 kwa makosa ya
wizi wa pikipiki 17 zilizoibwa katika maeneo mbalimbali ikiwiwemo
Gongolamboto na Tabata hivyo walikutwa na Sh Milioni 2.6
Aidha
amesema katika msako wamewakamata 216 wakiwa na dawa za kulevya
mbalimbali ikiwemo Bangi kilogramu 212, mirungi kilo 3.5 pamoja na kete
na misokoto ya Bangi na kukazia kuwa jeshi hilo linamshikilia Fatuma
Juma na wenzake 80 wakiwa mtambo wa pombe haramu ya Gongo.
Wakati
huo huo, jeshi hilo linamshikilia Joshua Kimange (66) kwa tuhuma za
kuawiti wataoto wenye chini ya miaka 7 katika eneo la Gongolamboto na
Kipunguni na kwamba mtuhumiwa huyo ameshafikishwa katika Mahakama ya
Kinyerezi.
Katika hatua nyingine, Kamanda
Muliro amesema wanamtafuta Godbless Sawe (47) kwa tuhuma za kumuua mkewe
Esther Benito kwa kutumia kitu chenye ncha kali eneo la Kibamba
wilayani Ubungo Juni 14 mwaka huu na kwamba baada ya tukio mtuhumiwa
alitoroka.
Kamanda Muliro amesema wanamshikilia
Frank Barnabas na mwenzake Joshua Shija kwa kujifanya askari polisi
ambapo walikuwa wakipita madukani kuomba misaada ya kutengeneza pikipiki
za polisi.
No comments:
Post a Comment