HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2022

Jiji la Dodoma latoa mikopo ya Sh bilioni 1.5

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


JIJI la Dodoma kupitia mapato yake ya ndani imetoa fedha za mkopo Shilingi Bilioni 1.5 kwa vikundi vya  wanawake 59 vijana 44 na Watu wenye Ulemavu 8 ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Jiji hilo.

Kupitia mkopo huo wa Shilingi Bilioni 1.5 Jiji la Dodoma limewakopesha vijana vyombo vya moto vya usafirishaji pikipiki na Bajaji Vikundi 15 vya vijana vyenye jumla ya wanachama 103, ambapo Bodaboda zilizonunuliwa ni 74 na Bajaji 14. Vitu hivyo vikiwa na thamani ya shilingi 387,000,000/=

Akizungumza kabla ya kumkalibisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru alimuagiza afisa Maendeleo ya jamii kuwaorodhesha wajasiliamali hao ili waweze kuwapatia viwanja kwa ajili ya kufanyia biashara kwani changamoto kubwa aliyoiona ni  kufanya biashara kwenye nyumba zao.

"Tumekuwa tukugawa viwanja lakini tumewasahau wajasiliamali wetu hivyo kuanzia Leo  naomba nipate orodha na nijue mahitaji yao ili tuwapatie viwanja kwa ajili ya kujenga ofisi za kufanyia biashara.

Aidha Mkurugenzi Mafuru aliwataka Wananchi wa mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo inayotolewa na Jiji kwani ni ukweli kwamba idadi ya watu wanaomba mkopo haiongezeki kila mwaka ni vikundi vile vile.

Alisena kumekuwa na maneno kwa baadhi ya watu kuwa hizi ni siasa hapana niwatoe hofu pesa zipo kwenye kata zenu mziombe ili kuweza kuwaibua kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na mkoa kwa ujumla .

"Kwanini tunatoa fedha hizi hapa tena kwa uwazi hivi uwezo wa kutoa kimya kimya Kwa kuwaingizia wajasiliamali wakiomba mkopo kwenye akaunti zao za benki tunao lengo letu la kufanya hapa kwa uwazi ni kuwajulisha Wananchi haya sio maigizo pesa zipo na hazina ukiritimba ombeni mtapewa

Kwa upannde wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri ambaye ndio aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo akiongea baada ya kuwakabidhi mkopo huo kwa vikundi hivyo vya wajasiliamali aliwataka wajasiliamali hao waliopatiwa mkopo kuhakikisha wanatumia mkopo huo kwa malengo lengwa ili iwe rahisi hata kulipa kwenye marejesho.

"Isije kutokea mmechukua mkopo halafu mnakwenda  kutumia fedha hizi nje ya malengo ni ukweli wazi mtashindwa kurejesha fedha hizi na ukianza kufuatiliwa utajihisi unaonewa Sasa sitaki tatizo hili lije litokee kwenu," amesema Shekimweri.

Aidha kwa Upande wa vijana waliokipeshwa pikipiki na Bajaji Mkuu huyo wa Wilaya aliagiza pikipiki na Bajaji waliokipeshwa zifungwe GPS ili kuweza kuwafuatilia na kuwatambua wanafanya shughuli ya usafirishaji au wanatumia vyombo hivyo kwa njia zisizo sahihi huku akiwataka vijana hao kuacha tabia ya Kutoa Saitimira na kutoa Pleti namba za vyombo vyo vya Moto kwa usalama wao

"Dhamira njema ya Serikali isiwaingize kwenye matatizo kumekuwa na taarifa baadhi yenu wamekuwa wakitumia pikipiki hizi kwa kufanya uhalifu huku wengine wamekuwa wakikimbia na Bajaji au pikipi na kuacha madeni yani kushindwa marejesho hivyo tukiwafungia GPS tutakuwa na uwezo wa kuwafuatilia na haitatokea mtu kuweza kukimbia na Chombo ," allisema Shekimweri

Naye Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana Si’gilinda Mdemu alisema akitoa taarifa ya hali ya urejeshaji katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 amebainisha kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya wakopaji kutorejesha mikopo kwa wakati.

"Pamoja na nia njema ya serikali lakini bado kumekuwa na changamoto ya vikundi kushindwa kurejesha kwa wakati hali inayosababisha  wengine kushindwa kupatiwa mikopo hii," alisema Mdemu

No comments:

Post a Comment

Pages