HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2022

TANESCO YAKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


NAIBU Mkurugenzi wa Uwekazaji Shirika la TANESCO, Peter Kigaje, amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kufanya tafiti  na kutengezeza mfumo wa kudhibiti hitilafu  ya Transfoma Janja ya mfumo wa umeme ambayo inakuja kutatua changamoto ya umeme hapa nchini.


Akizungumza katika kikao cha watafiti kati ya TANESCO na watafiti wa chuo kikuu cha Dar es salam ambapo alibainisha kuwa mfumo huo utaenda kulisaidia shirika la umeme hapa nchini.


"Imani yangu kuwa  Mfumo huu utakwenda kutatua matatizo yote ya kihandisi na nilikuwa natamani zaidi kuona Mfumo huo janja utakwenda kutatuliwa tafiti za kihandisi," alisema Kigaje.


 "Tatizo la umeme katika nchi yetu ni kubwa hivyo tafiti hiyo itaenda kutatua changamoto ya udhibiti wa italafu ya umeme kwani ni tatizo kubwa mfumo huo utaenda kuwa mwarobaini kwao,"alisema .


Aidha amesema chuo kikuu cha Dar es salaam kimekuwa na makubaliano ya mashirikiano na shirika la umeme nchini TANESCO na makuibaliano hayo yamekwisha muda wake lakini iko wazi  kuwa pamoja  kwa maana ya kuendeleza mahusiano kwa pamoja.


" Tumefurahi kuona chuo kinafanya tafiti kama hizi kwani mmeonyesha ni kweli mnafanya kazi na sio kuweka maandiko katika kabati hivyo basi sisi tunaimani maana tafiti hizi zitakwenda kutatua matatizo ambayo yapo katika jamii.


 "Mfumo huu wa Transfoma janja utakuwa na manufaa kwetu sisi kama shirika la umeme TANESCO kwani tunakwenda kuboresha mfumo na kuongeza ufanisi kwa wananchi na nchi kwa ujumla.


Kwa upande wake Makamu mkuu wa chuo cha Dar es salaam (UDSM) Bernadeta Killian alisema chuo hicho kimekuwa kikifanya tafiti, kufundisha, kutoa huduma kwa jamii bila kusahau kutoa ushauri ambapo akiendelea kueleza hata shirika la umeme TANESCO wamekuwa wakifanyanao kazi ya kutoa ushauri .


" Lakini tathimini zetu zimekuwa zikionesha kuwa hatufanyi vizuri kwenye kubadilishana maarifa na kwenye teknolojia na nipo tulipogundua kuna haja ya kufanya tafiti na huku tukijiuliza Ni tafiti za aina gani zinatakiwa kufanyika na ndio Maana tumekuja na tafiti hii kabambe.


Hata hivyo Projeti hiyo ilianza  mwaka 2015 huku wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ambapo changamoto nyingine zinaendelea kuwepo hadi leo hii.

No comments:

Post a Comment

Pages