Mgeni rasimi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri akizungumza na wanavikundi huku akiwasisitizia namna ya kwenda kuzitumia ili waweze kumudu kurejesha marejesho yao.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
VIKUNDI 59 vya wajasiriamali akina mama, vijana na watu wenye ulemavu vimepatiwa mkopo wa shilingi bilioni 1 5 na Jiji la Dodoma ikiwa ni asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani zinazotolewa na Halmashauri mbali na fedha hizo pia Jiji hilo limetoa pikipiki maarufu boda boda na bajaji.
Akizungumza wakati kumkalibisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Jabiri Shekimweri, Mkurugenzi wa Jiji hilo Joseph Mafuru amesema kuwa fedha zipo zinahutaji wakopoji waliofuata taratibu zote zinazotakiwa.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa anajua changamoto za wajasiriamali za maeneo ya kufanyia biashara zao kwani wengine wanafanya kwenye nyumba zao jambo ambalo halileti taswira nzuri kwa wafanyabiashara hao.
"Afisa Maendeleo ya jamii nakuagiza kuwaorodhesha wajasiliamali hawa ili waweze kuwapatiwa viwanja kwaajili ya kufanyia biashara kwani changamoto kubwa aniloyoiona ni ukosefu wa maeneo ya kufanya biashara ambapo kwa sasa kwenye nyumba zao," amesama.
Ameongeza kuwa wao kama jiji wamekuwa wakigawa viwanja lakini waliwasahau wajasiliamali hao na kuomba kupatiwa orodha ya mahitaji yao ili wapatie viwanja kwaajili ya kujenga ofisi za kufanyia biashara.
Aidha Mkurugenzi Mafuru amewataka Wananchi wa mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo inayotolewa na Jiji kwani ni ukweli kwamba idadi ya watu wanaomba mkopo haiongezeki kila mwaka ni vikundi vile vile
" Watu kumekuwa wakidhani hizi fedha tunazozitoa ni maigizo ndio maana tumekuja hapa ili wananchi wapate kujua kuwa hakuna maigizo naowaomba wananchi muende katika kata zenu kupata utaratibu wa kupata fedha hizi.
Kwa upannde wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Shekimweri ambaye ndio aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amewaomba wanavikundi hivyo kutumia mikopo yao kwa kusudio ili waweze kumudu kurejesha my mikopo yao
"Mtu anachukua mkopo halafu ana kwenda kutumia fedha hizi nje ya malengo mtashindwa kurejesha fedha hizi na ukianza kufuatiliwa utajihisi unaonewa sasa sitaki tatizo hili lije litokee kwenu," amesema Shekimweri.
Aidha kwa Upande wa vijana waliokipeshwa pikipiki na Bajaji Mkuu huyo wa Wilaya aliagiza pikipiki na Bajaji waliokipeshwa zifungwe GPS ili kuweza kuwafuatilia na kuwatambua wanafanya shughuli ya usafirishaji au wanatumia vyombo hivyo kwa njia zisizo sahihi huku akiwataka vijana hao kuacha tabia ya Kutoa Saitimira na kutoa Pleti namba za vyombo vyo vya Moto kwa usalama wao
"Dhamira njema ya Serikali isiwaingize kwenye mataitizo kumekuwa na taarifa baadhi yenu wamekuwa wakitumia pikipiki hizi kwa kufanya uhalifu huku wengine wamekuwa wakikimbia na Bajaji au pikipi na kuacha madeni yani kushindwa marejesho hivyo tukiwafungia GPS tutakuwa na uwezo wa kuwafuatilia na haitatokea mtu kuweza kukuimbia na Chombo ," allisema Shekimweri
Naye Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana Si’gilinda Mdemu alisema akitoa taarifa ya hali ya ujereshaji katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 amebainisha kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya wakopaji kutorejesha mikopo kwa wakati.
"Pamoja nania njema ya serikali lakini bado kumekuwa na changamoto ya vikundi kushindwa kurejesha kwa wakati hali inayosababisha wengine kushindwa kupatiwa mikopo hii," alisema Mdemu
No comments:
Post a Comment