HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 27, 2022

MOJA ya sababu za vifo vitokanavyo na uzazi ni utoaji mimba usio salama

 Na Irene Mark


Daktari Elias Kweyamba mtaalam wa afya ya uzazi na magonjwa ya wanawake, anasema kati ya asilimia 16 na 30 ya vifo vitokanavyo na uzazi husababishwa na utoaji mimba usio salama.

Anasema takwimu zinaonesha katika kila wanawake 100,000 kunatokea vifo 454 mpaka vifo 556 (Taarifa kutoka 2015/2016 TDHS). Vifo hivi visababishwavyo na utoaji wa mimba usio salama vinaonesha kuwa katika 16% mpaka 30%.


Suala la utoaji mimba usio salama limekuwa gumzo siku za hivi karibuni na takwimu zinaonesha vifo vitokanavyo na uzazi husababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo utoaji wa mimba usiosalama.

Takwimu zinaonesha katika kila Wanawake 100,000 kunatokea vifo 454 mpaka vifo 556 (Taarifa kutoka 2015/2016 TDHS). Vifo hivi visababishwavyo na utoaji wa mimba usio salama vinaonesha kuwa katika 16% mpaka 30%.

Utoaji wa mimba hauruhusiwi kisheria hapa Tanzania, Wizara ya Afya imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa miongozo ya baada ya mimba kuharibika (Comprehensive Post Abortion Care-CPAC) ili kuwaongoza watoa huduma za afya waweze kutoa huduma pale mimba inapokuwa imeharibika.

Kuna mimba nyingine zinatolewa kiholela kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo:

Mhusika kutokuwa tayari kulea ujauzito kwa wakati huo
Ukatili wa kijinsia kama ubakaji au baba au mtu wa karibu kumpa mimba mtoto wake wa kumzaa au ndugu wa karibu.

Mimba kwa mtu mwenye ulemavu mfano wa akili na hivyo kuongeza au kuchochea visa hivyo ambavyo husababisha vifo kuongezeka kila mwaka.

Siku za hivi karibuni Mbunge wa Viti Maalumu, Judith Kapinga aliongelea suala la utoaji mimba usio salama na kutoa baadhi ya takwimu na kuomba Waziri wa Afya kutoa muongozo kuhusu suala hilo Bungeni, Mei 30, 2022.

Mbunge huyu alieeleza kwa kina jinsi tunavyopoteza nguvu kazi nyingi kutokana na vifo vya wanawake vitokanavyo na utoaji wa mimba usio salama na hivyo kuomba wizara kutengeneza utaratibu ili huduma hii iweze kupatikana kwa utaratibu mzuri na salama.


Huduma ambayo mwanamke anatakiwa kuipata kitaalamu inaitwa Comprehensive Post Abortion - (cPAC) ambayo kwa Kiswahili inatambulika kama “Huduma Baada ya Mimba Kuharibika”, hii hutolewa kwa ajili ya kulinda usalama wa afya ya mwathirika wa tukio, wataalamu wa afya wanasema huduma huu ni muhimu sana kwa mwathirika.

Baadhi ya huduma za cPAC ambazo mwanamke anatakiwa kuzipata ndani ya muda mfupi tangu kuharibika kwa mimba au kutolewa ni:

-Kusafishwa kizazi (usafi wa kizazi), kupewa ushauri wa kisaikolojia, kupewa elimu ya afya ya uzazi
-Kukupewa dawa maalum, kupewa au kuongezewa maji, damu n.k
-Kuchunguzwa Saratani ya Matiti
-Kuchunguzwa magonjwa wa zinaa kama vile H.I.V au gono
-Kuchunguzwa magonjwa ya kuambukiza
-Kupewa ushauri wa afya ya kizazi na saikolojia
-Huduma ya kuchunguzwa Saratani ya Shingo ya Kizazi

No comments:

Post a Comment

Pages