Na Gasto Kwirini wa Jeshi la Polisi Arusha
Mkuu
wa Polisi Dawati la Jinsia na Watoto Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi
DCP Maria Nzuki leo tarehe 15.06.2022 ameongoza Maofisa, Wakaguzi na
Askari toka madawati ya jinsia na watoto Mikoa yote ya Tanzania kwa
ajili ya kutoa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto
mkoani Arusha.
DCP Nzuki
amesema kuelekea siku ya mtoto wa Afrika inayofanyika kitaifa wilaya ya
Simanjiro mkoani Manyara tarehe 16.06.2022 amesema wakiwa mkoani Arusha
watatoa elimu katika kata zote za Jiji la Arusha ikiwemo shule za
msingi.
Sambamba na hilo
amesema anaimani kuwa jamii itabadilika baada ya kupata elimu ya hiyo
kwani vitendo hivyo havikubaliki katika jamii na vinaadhibiwa kisheria.
Aidha
ametoa wito kwa Wananchi kubadilika ambapo amewataka kuwatunza watoto
wao na kukemea baadhi ya wazazi kuwaacha watoto wao bila ya uangalizi
ama kulelewa na wasichana wa kazi hali ambayo inapelekea vitendo vya
ukatili kuongezeka katika jamii.
Bwana
Mpeli Ally kalonge toka *SOS Children's Villages* ambayo ni taasisi
isiyo ya kiserikali amesema ukatili dhidi ya watoto unadumaza haki zao
na kuwa na madhara makubwa kwa maendeleo yao ambapo amesema wao kama
shirika wanaowajibu wa malezi ya watoto pamoja uimarishaji wa familia
kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na usalama
wa mtoto.
Kwa upande wa
Wananchi wa jiji la Arusha wamefurahishwa na elimu iliyotolewa ambapo
wamesema imewasaidia kujua kuwa watoto wote wana haki sawa katika kupewa
huduma mbalimbali.
Zaidi
ya Askari 90 wa vyeo mbalimbali ambao waligawanywa katika kata zote za
Jiji la Arusha walipata fursa ya kutoa elimu za ukatili katika mashule
na maeneo ya mikusanyiko.
No comments:
Post a Comment