HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 23, 2022

ACT WAZALENDO yahamasisha Sensa ya Watu na Makazi

Makamo Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Massoud Othman amesema  kuamua kwao kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar walikua na lengo likiwemo la kuikwamua Zanzibar katika hali mbaya ya kisiasa pamoja na uchumi.

 

Aliyasema hayo huko Tungu Mkoa Mkusini Unguja wakati akifungua Afisi mpya na ya kisasa ya chama hicho huko Tunguu Mkoa wa kusini Unguja jana (leo).

Alisema mambo yanayotokea hayatokei kwa bahati mbaya ni mamuzi ya  chama hicho kuingia katika serikali si ya kutafuta vyeo kama wengine walivyodhani hapo awali.

 

‘’Tulipoamua kuingia Serikali si kwa kubahatisha bali tulikua na ajenda zetu na ndio maana leo sasa kila mmoja anaona mambo yameanza kubadilika’’aliongezea.

 

Wakati akiendelea kunadi sera hizo Othman alisema kila mmoja ni shahidi jinsi Serikali ya Muungano  ikiongozwa na Rais Samia na kila mmoja ni shahidi jinsi mambo yanavyoendelea kubadilika.

 

Katika hatua nyengine Othman aliwataka wanachama wa chama hicho kujipanga zaidi kimageuzi na mabadiliko kwa kuwa ni sehemu ya dira ya chama hicho na hawanabudi kukubali mamabadiliko na kuajidaa.

 

Akizungumzia kuhusu hali ya uwajibikaji kwa viongozi waliopo Serikalini alisema viongozi hao wanapaswa kufanya kazi kwa bidii zaidi wakitambua wamekula kiapo cha uaminifu wanapaswa kufanya kazi muda wote kuonesha uwezo wao.

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, amewataka wanachama kushikama pamoja na kuunga mkono pia sensa ya watu na makaazi.

 

Amesema kushiriki kwao katika sensa kutawawezesha kuwa natakwimu sahihi na kuweza kufanya kazi za chama ikiwemo kuandika ilani ambayo itakidhi idadi halisi ya wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

 

Katika hatua nyengine Naibu huyo amesema harakati za Chama hicho zinaendelea kama kawaida kwa mujibu wa sheria na taratibu na kuwataka wananchama  wa chama hicho wajiamini katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

 

Mapema Katibu wa habari na Uenezi Chama hicho Salim Bimani alisema kufanyakazi kwa ufanisi kwa mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaotaka katika chama hicho ni kutokana  misingi imara aliyoijenga Makamu wa kwanza wa kwanza Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad katika enzi ya utawala wake.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Omar Said Shaban amesema Chama chao ni mbadala wa CCM na wapo tayari kushika dola na kuiongoza nchi nzima.

 

Alifahamisha katika hali isiozoeleka kwenye mkoa huo Chama Chao kimekua kikikuwa kila leo na kuongeza idadi kubwa ya wanachama katika ngome kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM.

 

Kufunguliwa kwa ofisi mpya ya chama na ya kisasa katika mkoa wa kusini Unguja ni mwendelezo wa harakati za kisiasa huku kukitarajiwa ofisi nyengine zaidi kujengwa na kufunguliwa kabla ya kufika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

No comments:

Post a Comment

Pages