Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Francis Maiko (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Warda Hamduni ambaye amebuni kifaa cha kieletroniki ambacho kinamuwezesha mtumiaji wa gesi za majumbani kujua kiwango cha matumizi yake. 'Gas Consumption Monitoring System'.
Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Maiko amekipongeza Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuwa na bunifu za kisasa ambazo zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali katika Jamii.
Dkt. Francis amesema hayo wakati alipotembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia na kuzungumza na wabunifu wa Chuo hicho kwa kusema kuwa bunifu zao ni muhimu kwa Taifa, hivyo lazima ziendelezwe.
" Chuo kinafanya kazi nzuri na hii inaonesha kuwa ni namna gani Chuo kimepiga hatua katika masuala haya ya ubunifu, nawapongeza sana, zamani tulizoea kuona taasisi chache zinazofanya bunifu lakini hivi sasa Chuo hiki kinepiga hatua kubwa sana katika masuala haya ya ubunifu,"alisistiza Dkt Francis.
Chuo hicho pamoja na kutoa kozi mbalimbali katika mwaka mpya wa masomo 2022/23 Kitaanza rasmi ufundishaji wa kozi mpya ya masomo ya Uongozi, Maadili na Utawala bora kwa ngazi ya Cheti, Diploma, Shahada na Shahahada ya Umahiri.
Dira ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni kuwa kitovu cha utoaji wa Maarifa bora kwa kutoa Elimu na Mafunzo kuhusu Ubunifu na uvumbuzi sambamba na kuendeleza Amani na Umoja wa Kitaifa.
Chimbuko la Chuo hicho ni Chuo cha kivukoni ambacho kilianzishwa rasmi Julai 29, 1961 na uamuzi wa kuanziahwa Chuo hicho ilikiwa ni uamuzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha TANU uliofanyika Tabora mwaka 1958.
Katika mwaka 1972 hadi 1992 Chuo hicho kilikuwa Chini ya Chana cha Mapinduzi CCM na kilimuwa na Vyuo vya Kanda 8 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maonesho hayo ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yalianza Julai 18 hadi Julai 23,2022 ambapo Wanafunzi wanaomba nafasi za kiunga na Chuo walidahiliwa moja kwa moja mara tu walipofika kutembelea banda hilo la Chuo.
Kauli mbiu ya monesho hayo ni Elimu ya Juu inayokidhi Mahitaji ya soko la Ajira, kwa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.
No comments:
Post a Comment