Na Mwadishi Wetu
Taasisi ya Uendelezaji kilimohai Afrika (AfroNet) imesema Tanzania ni miongoni mwa nchi nne zinazofanya vizuri kwa kuwa na wazalishaji wengi wa Kilimohai.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kuhusu mradi wa Bunifu za Kitaasisi kwa ajili ya Kilimohai Afrika (IIABA) Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya Kuendeleza Kilimohai Barani Afrika (AfrONet), Constatine Akitanda alisema ripoti ya mwishoni mwa mwaka jana inaonesha Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa wazalishaji wengi ikiongozwa na india, Uganda na Ethiopia.
Alisema kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa mwaka jana na taasisi ya kimataifa ya Utafiti wa kilimohai (FiBL), Kidunia kuna wazalishaji milioni 3.1 wanaozalisha chakula chenye ubora.
“Kiwango cha ukuaji wa wastani wa sekts hiyo ni asilimia 9.5 na Hekta zinzolimwa kidunia ni milioni 72.28 kuonesha namna kuna wingi wa chakula ingawa kuna tofauti katika ubora”
Alisema uwapo wa AfroNet utasaidia kutafuta majawabu ya kudumu katika kutafuta chakula yanayoweza usalama wa lishe.
Akitanda alisema kuna changamoto hasa kwa wazalishaji ambao baadhi wamekuwa wakitumia kemikali katika mashamba bila utaalamu.
“Tunataka wananchi a=Afrika nzima waelewe athari za matumizi ya Kemikali na njia ya kuepuka kutumia na kufanya uamuzi sahihi wa uzalishaji “ Alisema.
Akizungumza kuhusu mradi huo tangu kuzinduliwa mwaka juzi, walikuwa wakiangalia namna ya kuchagiza maendeleo ya ukuaji wa kilimohai, kuangalia njia sahihi, kuibua ubunifu na kujengea uwezo taasisi, na mamlaka za serikali na wadau mbalimbali na kuibua masoko.
Alisema mradi huo ambao unatekelezwa kwa ushirikiano na na shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unagusa nchi tatu za Tanzania, Uganda na Morocco. Tnagu uzinduliwe umefikia asilimia 45 ingawa uliathiriwa mlipuko wa Covid-19.
Akitanda alisema mradi huo umesaidia Uganda kufanikisha sera ya Kilimo hai na kwa sasa inasambazwa kwa wannchi na huku wakiendelea na mkakati wa kuandaa sheria ya kusimamia utekelezaji. Alisisitiza kuwa Tanzania inafanya vizuri Kisera.
Naye mratibu wa mradi huo Mgeta Daudi alisema Uganda wako vizuri katika masoko kwani wameanzisha vikundi shirikishivya kusimamia bidhaa za kilimohai.
Morocco ambao pia ni wanufaika, wanatajwa kuwa wameanza kuinuka baada ya kuonekana wakisuasua.
Alisema mpango uliopokwa AfroNet ni kuazisha masoko ya Kilimohai baadhi ya mikoa, hususani Dodoma na Zanzibar, kuandaa mikutano itakayokutanisha wadau wa Sekta hiyo duniani.
No comments:
Post a Comment