HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2022

GCLA yasisitiza matumizi salama ya kemikali

Mkemia Mkuu wa Serikali, Fidelice Mafumwiko (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.

 

Na Irene Mark

MKEMIA Mkuu wa Serikali, Fidelice Mafumiko, amewataka wananchi kutafuta kupitia ofisi za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), taarifa sahihi kuhusu matumizi salama ya kemikali kwenye shughuli mbalimbali.

Mafumwiko amesema hayo leo Julai 07,2022 wakati akitoa maelezo kuhusu matumizi sahihi ya kemikali kwa wananchi waliotembelea banda la mamlaka hiyo.

Amesema GCLA inasimamia uingizaji na kudhibiti kemikali zinazoingia na kutumika hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha inatumika vizuri bila kuleta athari kwa mtumiaji na mazingira.

“Kemikali ina faida nyingi ukiitumia kwa usahihi inavyostahili lakini ukiitumia visivyo athari zake ni kubwa na mbaya mno.

“Ndio maana tunawaambia wananchi hasa wafanyabiashara wapite kwenye banda letu tuwape elimu sahihi ya matumizi ya kemikali.

“Kama kama kauli mbiu ya maonesho ya sabasaba mwaka huu inavyosema Tanzania ni pahali salama kwa kuwekeza  hivyo wenye viwanda, wafanyabiashara wanaotumia kemikali wahakikishe wanaitumia kwa usahihi bila kuleta athari kwa watumiaji,” amesema Mafumwiko.

Amesema kemikali zinamatumizi makubwa viwandani na kwenye biashara hivyo lazima itumike kwa usahihi.

Mafumwiko alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kufuata taratibu katika kupima vinasaba (DNA), huku akisisitiza kwamba Serikali inagharamia vipimo hivyo kwa sehemu kubwa.

“Ki uhalisia gharama ya kupima vinasaba ni kati ya sh. 700,000 na sh. 800,000 kwa mtu mmoja lakini ofisi yake inatoza sh. 100,000 kwa mtu kwa kuwa tayari serikali imewekeza hivyo mwananchi anachangia kidogo,” amesisitiza Mafumwiko.

No comments:

Post a Comment

Pages