Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Uchimbaji Gesi na
Mafuta (OGAWOGA), Frank Mwankefu akizungumza na waandishi wa habari
namna PURA ilivyosaidia wao kuaminika na kupata kazi kwenye makampuni ya
uchimbaji na uzalishaji gesi asilia, alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Viwanja vya Sabasaba wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.
Mhandisi wa Petroli Alexander Gosbert akitoa elimu kwa watawa wa Kituo cha Wadada Wadogo kwenye banda la PURA katika walipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Viwanja vya Sabasaba wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.
Na Selemani Msuya
UTELELEZAJI
wa Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG), katika mikoa
ya Kusini mwa Tanzania utachochea ukuaji wa uchumi, maendeleo na huduma
za kijamii kwa wananchi na mikoa hiyo.
Mradi huo ambao uwekezaji wake unatarajiwa kuanza mwaka 2025 mkoani Lindi na kukamilika 2030 unagharimu Sh.trilioni 70.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika Banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa
Juu wa Petroli (PURA), lililopo Viwanja vya Julius Nyerere maarufu
Sabasaba Temeke jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Halfani
Halfani alisema mradi wa LNG unaenda kufanya mapinduzi kwa wananchi
mikoa ya Kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na Pwani.
Halfani
alisema mradi wa LNG ukitekelezwa kwa kiwango ambacho kinarajiwa gesi
nyingi itazalishwa na kutumika nchini na nyingine kuuzwa nje hivyo
kuongeza ajira.
"Katika
utelelezaji wa mradi huu ajira zisizo za kudumu zaidi ya 10,000
zitapatikana.Mfano wauza nondo, saruji, kokoto, vyakula na vingine,
hivyo mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa na mapinduzi ya kiuchumi na jamii
yataonekana,"alisema.
Halfani
alisema PURA itaendelea kutafuta wawekezaji ambao watawekeza katika
eneo la mafuta na gesi ambalo limeonesha mafanikio makubwa katika kuinua
uchumi wa nchi nyingi.
Alisema
pia PURA inaendelea kuunganisha kampuni za Kitanzania ambazo
zinazotaka kushiriki utafutaji na uchimbaji gesi na mafuta kupata
nafasi.
Mwenyekiti
alisema uamuazi wa Serikali kuruhusu uchimbaji wa gesi asilia umewezesha
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwa na uhakika wa nishati ya
umeme na ambao unatumiwa na wananchi wengi mjini na vijijini.
Alisema pia wanahamasisha wananchi kutumia gesi asilia majumbani kwa kuwa ni salama kwa wananchi.
"Mimi
nasisitiza majadiliano yaendelee kuwa mazuri, ili lengo la Serikali
kuzalisha gesi asilia ya LNG yafanikiwe kama yalivyopangwa," alisema.
Aidha
alisema PURA imekuwa ikishawishi Watanzania kushiriki kwenye miradi
mbalimbali ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi ambao mwitikio
umeanza kuonekana.
Kwa
upande wake Mkuu wa Operesheni wa Kampuni ya Solution Tag Consultant
Limited, Tumain Abdallah alisema PURA imekuwa kiungo muhimu wa wao
kupata kazi kwenye miradi ya uchakataji gesi asilia.
Abdallah
alisema kwa muda mrefu kampuni za wazawa zilikuwa haziaminiki ila
kupitia PURA wameaminika na kupewa kazi za ushauri wa masuala ya mafuta
na gesi.
"PURA
imewaaminisha wawekezaji kuwa sisi tunaweza na hatujawaangusha, kwani
tunaendelea kutoa huduma za masuala ya gesi na mafuta kwa kiwango
kikubwa,"alisema.
Alisema
kampuni yao ina wafanyakazi wazawa tisa ambapo ameshauri vijana
Wakitanzania ambao wamesoma mambo ya gesi na mafuta kujitokeza
kushiriki.
Naye
Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Uchimbaji Gesi na Mafuta (OGAWOGA), Frank
Mwankefu alisema ujio wa PURA umeweza kuwafanya watambulike na kupata
kazi katika miradi ya Songo Songo na kwingine.
"Hii PURA imetufanyia mambo makubwa sisi wachimbaji wa mafuta na gesi, tunaahidi kutowaangusha," alisema.
No comments:
Post a Comment