Na Talib Ussi, Zanzibar
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar Joseph Kilangi
ameahidi kusitisha mkataba na Kampuni ya Simba Developa inayojenga mradi
wa tangi la Kuhifadhia Maji Safi na Salama eneo la Mgeni Haji Wilaya
ya Maghari A Unguja, kwa kutoridhishwa na utendaji kazi wa kampuni
hiyo.
Aliyasema hayo
wakati alipofanya ziara yake ya kiutendaji ya kukagua miradi ya Maji
Safi na Salama inayotekelezwa na kampuni mbalimbali ikiwemo kampuni ya
Afcon, Simba Developa na Shanjo.
Alisema
utekelezaji wa kampuni hiyo (Simba Developa) haujafikia hata asilimia 30
ya ufanyaji kazi, hivyo endapo ujenzi huo utaendelea kudorora, atashauriana na mwasheria wa wizara yake ili kuandaa utaratibu wa kusitisha mkataba pamoja na kuwatoza fidia kampuni hiyo.
“Mradi
wa ujenzi la tangi ni mradi wa miezi minane lakini hadi sasa miezi
minne imepita wamechimba shimo na kufunga nondoo chini basi! hakuna kazi
inayoendelea hatuwezi kuendelea na kampuni hiyo, nitakaa na mwasheria
kuangalia namna ya kuvunja mkataba na kuwatoza faini wailipe serikali
kwasababu wameshatupoteza muda, serikali haitoweza kufanya nao kazi
tena” Alisema Kilangi
Alisema
hatua ya kukatisha mkataba itafanyika kwa kampuni zote ambazo
zitashindwa kutimiza ahadi kama waliyokubaliana, na kila kampuni ina
muda waliyokubaliana katika kutekeleza mradi, hivyo hakuna kuongeza
muda.
Alielezea Mradi wa
Maji unayotekelezwa na kampuni ya Afcon kupitia fedha za Exim Benki
ambapo ni mkopo nafuu wa dola milioni 92.18 unajukumu la kuchimba
visima, kujenga matangi ya kuhifadhia maji, kufukia maboba pamoja
kujenga nyumba ya kuhifadhi Maji (Maji House) unaendelea vizuri.
Katika
hatua nyengine Katibu Mkuu huyo alitembeleza kisima cha Maji katika
Kijiji cha Bumbwisudi ambapo ameridhishwa na utekelezaji wa kisima
hicho, nakusema kwamba kisima hicho kitapoanza kutumika tatizo la maji
litakua historia kwa mji wa Zanzibar.
Alisema
kisima hicho kinauwezo wa kusukuma maji lita laki mbili na hamsini
(250,000) kwa muda wa saa moja kwa mujibu wa wataalam ambapo maji hayo
yatapelekwa katika tangi la Welezo na kusambaza Wilaya ya Mjini Unguja.
Kilangi
pia alitembelea mradi wa maji unaotekelezwa na kampuni ya Shanjo
kupitia fedha za ahuweni za UVIKO-19 katika Shehia ya Mbuzini Wilaya
Magharibi ‘A” wenye thamani ya dola bilionii 34.2 ambapo ameridhishwa na
utekelezaji wake na kuwasisitiza wataalam kuongeza kasi ya utendaji.
Naye
Meneja Mradi bw. Rashid Mohamed kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar
(ZAWA), alisema mradi wa kisima kupitia fedha za ahuweni za UVIKO-19
unajukumu la kujenga matangi 10 kwa Unguja na Pemba, kuchimaba visima
vipya 38 pamoja kufanya kazi ya kutandika mabomba.
Alisema
mara tu vifaa vitakapoingia nchini Julai 15, mwaka huu hakuna sababu ya
kuchelewesha kazi kwasababu timu ya wataalum iko imara kiutendaji.
Kwa
upande wake Mhandisi Hassan Khamis Hassan ambae ni Mkurugenzi ZAWA,
alisema Kisima cha Bubwisudi hakina tatizo kimefungwa mashine kubwa ya
kusukumia maji ila wanahitaji usalama wa mashine hiyo na wameshafanya
utaratibu wa kuwaomba ZECO wasaidie kifaa hicho cha usalama wa mashine
(mota).
Mapema Mhadisi wa
kampuni ya Simba Develop Hassan Hamad, alisema utekelezajwi wa mradi wa
tangi la maji kupitia kampuni hiyo unatokana na mshauri elekezi ambapo
alifelisha kokoto zilizoagizwa mwanzo kutona na ardhi ya hapo ina maji
maji isingeweza kukidhi vigezo vilivyohitajika lakini tayari
wameshaagiza kokoto zinanostahiki na kuendelea na kazi.
Ziara
ya katibu Mkuu Kilangi ni ziara ya siku mbili, ambapo siku ya kwanza
alitembelea Mradi wa maji shehiya ya Masingini, Dimani, Nyumba ya
kuhifadhia maji eneo la Miembeni ( Madema) ambapo shughuli hizo
zinatekelezwa na fedha za Exim Benki.
Pia
alitembea mradi wa maji Mbuzini unaotekelezwa kwa fedha za ahuweni za
UVIKO-19 na mradi wa ujenzi wa tangi la kuhifadhia maji Mgeni haji
linalojengwa na kampuni ya Simba Developa.
No comments:
Post a Comment