HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 19, 2022

KATIBU MKUU KILANGI AWATAKA WATENDAJI KUWAJIBIKA

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji , Nishati na Madini Joseph Kilang akizungumza  na wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa lengo la kuboresha utendaji kazi. 

 

Na Talib Ussi, Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph Kilangi amewataka watendaji wote wa wizara hiyo kuwajibika katika kuwahudumia wananchi kupata huduma ya Maji Safi na Salama, Nishati na Madini ili kuwaondolea usumbufu wanaoupata  katika kupata huduma hizo hasa Maji.

Aliyasema hayo katika ukumbi wa ZURA wakati akizungumza na watendaji hao kwaajili ya kuboresha utendaji kazi wa wizara anayoisimamia ili kupunguza malalamiko ya huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Zanzibar.

Alisema Maji yanaweza kupatikana kila kona ya Zanzibar lakini anashangazwa kwanini watu hawapati maji huenda kuna watu wanafunga maji kwa makusudi ili watumia magari kwaajili ya kufanya biashara ya maji huku wananchi wakiteseka jambo ambalo sio sahihi hata kwa Mwenyezi Mungu.

“Kila mfanyakazi ndani ya wizara hii akiulizwa nafasi yake ya kazi aseme mimi nawatumikia wananchi kupata huduma ya maji kwa hiyo mfanyakazi yeyote atakayemuona mtu anafunga koki ya maji basi atowe taarifa kwa kiongozi wake haiwezikani watu wakosema maji, Mtu akipiga simu maji yanfunguliwa ni wazi kama kuna mchezo unachezwa! Suala la maji linaniumiza kichwa” Alisema Kilangi.

Katibu Mkuu Kilangi aliwataka watendaji hao kila mmoja kuwajibika katika majukumu aliyopewa bila ya kusubiri kusukwa na uongozi kwasabau kila mfanyakazi apewa majukumu yake (Job Description). Alisema kinachohitaji katika kutekeleza majukumu hayo ni mashirikaina ya karibu ndio yatakayoleta maendeleo katika wizara hiyo.

Aidha alimuagiza Mkurugenzi Utumishi na Uandeshaji kufunga mfumo wa alama za zidole haraka iwezekanavyo ili kuangalia kwa karibu mahuduria wa wafanyakazi kwani nidhamu inaanza na mahudhuri ya mfanyakaza wakati wa kuingia na kutoka kazini.

“Sitaki kusubiri ripoti ya makaratasi nitazidiwa akili nataka ikifika mwisho wa mwezi na print biometric system inioneshe kwa jina mfanyakazi aliingia saa ngapi kama saa 2.30 au saa 3.00 na muda aliyotoka. Nahao wasio sikia Mkrugenzi Utumizi watwange barua kama mtu umemwita hataki kusikia mpe barua, hatukusudii kuharibiana lakini kama mtu hataki kubadilika basi sheria za utumishi zitumike. Alisema Kilangi.

Naye Naibu katibu Mkuu Mwanajuma Majid Abdalla alisema kama wanananchi hawapati huduma ya maji basi wizara hii itakuwa haina uwajibikani hasa ukiangalia huduma hii ni muhimu sana kwa kila mtu kwani bila ya maji hakuna mtu atakaweza kuishi.

Alisema wafanyakazi msiridhike ma majibu ya mafundi ya kusema maji hayatoki, bila ya

kueleza sababbu ya msingi kwasababu kunawatu wanancheza na akili za watu utadhani hawajui kama huduma ya maji inathawabu.

No comments:

Post a Comment

Pages