HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 12, 2022

MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA PSSSF DKT. AGGREY MLIMKA AFURAHISHWA NA MATUNDA YA UWEKEZAJI WA MFUKO HUO

MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Dkt. Aggrey Mlimuka ametembelea banda la USHIRIKIANO linalotumiwa na Mfuko huo na ule wa NSSF kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam na kujionea matunda ya uwekezaji katika kiwanda cha kuchakata Tangawizi kilichoko Mamba Miamba, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
 
"Kwakweli ni hatua nzuri ni jambo la kufurahisha sasa tumeona matokeo, nimeona matunda ya uwekezaji, tangawizi hii ni nzuri yanahitajika marekebisho kidogo kwenye vifungashio lakini ina ubora wa kuuzwa hata nje ya nchi." Alisema Dkt. Mlimuka.
PSSSF imewekeza kwenye kiwanda hicho cha kuchakata Tangawizi kwa ushirikiano na Wanaushirika wa Mamba Miamba Wilayani Same.
 
Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28 yanatarajiwa kufikia kilele Julai 13 na yanakwenda na kauli mbiu isemayo "Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji."
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini PSSSF, Dkt. Aggrey Mlimuka (wapili kushoto) akisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo, Bw. James Mlowe (wakwanza kushoto) kuhusu tangawizi iliyochakatwa inayozalishwa na kiwanda cha Tangawizi Mamba Miamba kinachomilikiwa kwa ubia baina ya Mfuko na Wanaushirika wa Mamba.

Bw. Kijazi akisindikizwa na Meneja wa PSSSF, Zanzibar Bi. Amina Kassim
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala PSSSF Bw. Paul Kijazi (kulia) akipatiwa maelezo na Afisa Uhusiano Mkuu PSSSF, Bi. Fatma Elhady kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko kwenye banda la PSSSF.
Bw. Kijazi (kushoto), akizungumza na Afisa Uhusiano Mwandamizi PSSSF, Bi. Rehema Mkamba wakati akiondoka kwenye banda la Mfuko baada ya kulitembelea.
Mkurugenzi wa Takwimu,Uthamini na Hadhari ya Majanga Bw. Ansgar Mushi (kulia), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko aliyetembelea banda PSSSF Julai 11, 2022
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini (PSSSF) Dkt. Aggrey Mlimuka (kushoto), akimsikilzia Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, PSSSF, Bw. James Mlowe wakai Dkt. Mlimuka alipotembelea banda la Mfuko huo JUlai 11, 2022. Kulia ni Meneja wa PSSSF huko Zanzibar, Bi. Amina Kassim. 

No comments:

Post a Comment

Pages