Na Mauwa Mohammed Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Husein Ali Mwinyi amesema suala la kuwashughulikia na kuwatunza watoto yatima ni jambo jema sana mbele ya mwenyezi Mungu.
Alisema kwani watoto hao huwa wanapambana na changamoto nyingi katika maisha yao na wamapopata watu wa kuonyesha huruma kwa kuwapatia huduma hujisikia faraja.
Kauli hiyo ameitoa katika hafla ya dua na dhifa ya chakula cha mchana na watoto yatima kwa kusherehekea sikukuu sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Maos tung Mjini Zanzibar.
"Nawahimiza wananchi tutekeleza wajibu wetu wa kuwalea watoto yatima na kujenga mahusiano mema kwao ili wahisi hawako pekeyao" alisema Dk. Mwinyi .
Aidha alisema ipo haja ya kuratibu vizuri watoto yatima na kuhakikisha kila kinachotolewa kinawafikia wote na sio wachache.
Alisema kwani kumekuwepo na asasi zenye kushughulikia yatima lakini hazifikii malengo, hivyo kuna haja ya kuratibu vizuri na kuhakikisha kila kinachotolewa kinawafikia yatima wote.
Sambamba na hilo aliwahimiza walimu kuhakikisha wanaweka mazingira malum ya watoto hao ili kuwaondoshea huzuni na shida zinazowakabili.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Nuru Fondation inayoshughuilikia watoto hao Bi Zainab Kombo alisema ipo haja ya kuhamasisha na kuona juhudu za kuchangia ili kuwashughulikia watoto Yatima hasa wanaoishi katika mazingira magumu.
Alisema lengo ni kuwaweka katika upendo watoto hata wasiokuwa Yatima lakini na wale wanaonekana wanaishi katika mazingira magumu.
Hatua hiyo ya kuwachangia watoto Yatima imeandaliwa na Jumuiya inayoshughulikia watoto Yatima Nuru Fondation kwa kushirikiana na jumuiya ya Zardefo, Muzdalfa na Jumuiya mama ya wanawake wa Kislam.
No comments:
Post a Comment