Zaidi ya waleta mabadiliko 50 wa mashirika ya kiraia walihudhuria kongamano hilo. Miongoni mwao alikuwa Bi. Rose Nzali kutoka IOGT-NTO Movement EA. Bi Rose akiguswa na mawasilisho ya nguvu ya utoaji, na shuhuda juu ya athari iliyonayo, alichukua hatua ya kuchangia kwa Doris Mollel Foundation, huku akiwahimiza washiriki wengine waliohudhuria kuchangia pia.
Mwishoni mwa Kongamano hilo, Karin Rupia kutoka FCS, alishauri waliohudhuria kongamano hilo kujitokeza na kushughulikia masuala yanayohitaji msaada katika jamii zetu kwa kutumia zana ambazo tayari watu wanamiliki. Pia aliwasihi wahudhuria kujumuisha wanafamilia na marafiki zao katika harakati za kutoa misaada. Alisema hivi kuwasilisha kwamba uhisani, kujitolea na/au uchangiaji sio tu kuhusu kutoa rasilimali za kifedha bali ni kutoa nguvu na uwezo wako pia - kwasababu aina yoyote ya juhudi ndogo zinazowekwa katika kutoa msaada huleta mabadiliko makubwa.
No comments:
Post a Comment