HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2022

NANDY AFUNGUKA KUHUSU UJAUZITO WAKE

Msanii wa Bongofleva Nandy ambaye kwasasa ni mama kijacho, akitarajia kupata mtoto wake wa kwanza na Rappa BillNass hivi karibuni, usiku wa kuamkia leo kulikuwa na sherehe ya ‘kitchen party’ yake ambapo kwa mara ya kwanza aliweza kuzungumza na mwandishi wa habari na kueleza machache kuhusiana na ujauzito wake.


Kwenye mahojiano hayo na mtangazaji wa Sherehe Zetu ambao ndio walikamilisha shughuli nzima ya sherehe hiyo, Nandy amesema, mumewe mtarajiwa (Billnass) ndio wa kwanza kugundua kuwa yeye ana ujauzito mara baada ya kuona mabadiliko mbalimbali kama ya kitabia.

Pia amebainisha kitu alichokuwa akikitamani ni kupata mtoto akiwa tayari yupo ndani ya ndoa, hivyo kwa namna ilivyotokea amesema ni baraka pia.

"Nilikuwa natamani kupata mtoto nikiwa tayari nipo ndani ya ndoa. Nimejaliwa nikiwa bado sijaingia kwenye ndoa lakini huyu mtoto ntaingia nae kwenye harusi na kwenye ndoa hivyo sio kitu kibaya ni baraka na wazazi wote wameridhia" - ameeleza Nandy.

Ikumbukwe, Nandy na Billnass wanatarajia kufungua ndoa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Pages