Na Julieth Mkireri
MKuu Wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amepokea ng'ombe 500 pamoja na mbuzi 1000 kutoka katika Taasisi ya Iddef ya Uturuki kwa ajili ya kugawia makundi yenye uhitaji kwenye Sikukuu ya Eid.
Msaada huo ulioutolewa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rahma Foundation una lengo ya kuwezesha wananchi wenye uhitaji kushiriki sikukuu hiyo kwa kuchinja kama ilivyo kwa wengine wenye uwezo.
Kunenge amesema ng'ombe hao watachinjwa na kugawanywa kwa watu wenye mahitaji wakiwemo yatima wajane na wazee katika mkoa huo.
"Tutasimamia kwa uadilifu tutatumia utaratibu kushirikiana na Bakwata mkoa wa Pwani na viongozi wa dini naamini hili litaenda vizuri na walengwa watafikiwa" amesema.
Aidha kunenge ameishukuru Taasisi ya iddef kwa kuwezesha wananchi hao kusherekea kwa kupata kitoweo hicho kama yalivyo makundi mengine yenye uhitaji ambapo aliwaomba kwa mwaka ujao kutoa msaada kama huo kwa makundi yenye uhitaji.
Mwakilishi wa Taasisi ya Iddef Ahmad Furqan amesema wana nchini 40 wanazihudumia waislam na wasiokuwa Waislam.
Amesema Taasisi hiyo kutoka Uturuki imeundwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye uhitaji kwenye nchi mbalimbali.
Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia Taasisi hiyo na kutoa huduma na misaada kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Naye mwakilishi wa Shekhe mkuu wa Mkoa wa Pwani Salmin Buda ameshukuru Taasisi hiyo kwa msaada walioutoa huku akimuahidi Mkuu wa Mkoa kushiriki kikamilifu kugawa msaada huo kwa makundi yaliyolengwa.
No comments:
Post a Comment