HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 21, 2022

Nandy Balozi wa Bima kampuni ya Assemble


Meneja Mauzo wa Assemble Insurance, Arthur Mndolwa (wa kwanza kulia), Meneja Maendeleo na Mahusiano ya Assemble Insurance, Mwamvita Said (mwenye kilemba cheupe) wakiwa na Balozi wa Assemble Insurance, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).

 

 Na Irene Mark

KAMPUNI ya Bima ya Assemble, imemtambulisha msanii wa muziki wa kizazi kipya Faustina Mfinanga ‘Nandy’ kuwa Balozi wake na kupata huduma ya bima ya afya.

Nandy au African Princess ambaye kwa sasa ni mjamzito atanufaika na fao la afya ya uzazi la juu kabisa la Gold Cover linalofikia Sh. milioni 200 kwa mwaka na kupatiwa huduma yeye, mume wake na mtoto wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 20,2022 wakati wa  kumtambulisha balozi Nandy, Meneja Mauzo wa kampuni hiyo nchini, Authur Mndolwa alisema pamoja fao hilo la Gold yapo pia mafao mengine ya silver na Bronze yenye gharama nafuu yaliyolenga wananchi wa kada na rika zote kiuchumi.

"Kampuni yetu inamthamini kila mteja na ndio maana tuna fao ambalo litamuwezesha kila mtu kunufaika kulingana na gharama anayomudu. Fao letu la bima ya afya la chini kabisa ni kuanzia shilingi 350,000 hadi 450,000 na mtu ananufaika hadi shilingi milioni 5.5," alisema.

Alisema bima hiyo ya afya ambayo Nandy ni balozi wake ina mafao mengi ikiwemo kupata huduma kabla na baada ya uzazi, huduma za lishe bora, mazoezi na huduma ya saikolojia.

"Lakini pia kupitia bima yetu hii anaweza kutibiwa popote nchini kwani tunafanyakazi na vituo vya afya 150 nchini kote na Afrika nzima na Hospitali kubwa kama Appolo nchini India," alieleza.

Alisema kampuni hiyo pamoja na kuwa na bima ya afya ambayo wana wanachama takribani 40,000 nchi nzima pia inatoa bima mbalimbali kama vile za vitu, mali, mali na maisha.

"Assemble Insurance inajivunia uhodari wao wa kutoa huduma za bima takribani zaidi ya miaka 35 kwa Tanzania na Afrika. Na katika kuhakikisha hilo Assemble inaushirika na  Hospitali zaidi ya 600 nje na ndani ya Tanzania," alibainisha.

Kwa upande wake, Meneja Maendeleo na Mahusiano wa Assemble Insurance Mwamvita Said alisema kampuni hiyo ina kauli mbiu inayosema kesho yako wanailinda.

Alisema kesho hiyo wanailinda kwa kuendelea kuunga mkono sekta ya bima ya afya na kuhakikisha kila mtanzania anaweza kufaidika na fao la bima hasa la mama na mtoto.

"Katika kuhakikisho hilo Assemble Insurance wameweza kuanzisha bima inayo fahamika kama Bronze Jamii ambayo inapatikana kwa gharama nafuu zaidi ," alisema Mwamvita.

Naye, Nandy aliishukuru kampuni hiyo kwa kumpatia ubalozi na bima hiyo inypmuhakikishia afya yake hususani katika kipindi hiki anachotarajia kupata mtoto.

Aliwatoa wasiwasi mashabiki wake kuhusu tamasha lake la Nandy Festival kwani Assmble Insurance imehakikishia kuwa kwa asilimia 100  itahakikisha anafanya show, ikiwa tayari madaktari wamejiridhisha kuwa yeye na mtoto wake afya zao ziko salama zaidi.
 

No comments:

Post a Comment

Pages