- Aelekeza Barabara kuu kusafishwa na kufungwa mifumo ya umwagiliaji.
- Asisitiza Upandaji miti na bustani za watu kupumzika.
- Viongozi wa Machinga wajitolea kuisaidia Serikali kuwapanga vizuri Machinga Wanaofanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla ametangaza Operesheni kabambe
ya Usafi wa Barabara kuu za Mkoa huo ifikapo Jumamos ya Julai 30 ambapo
ameelekeza Wananchi na Wakandarasi wa Kampuni za uzoaji wa taka
kushiriki kwenye zoezi Hilo.
RC
Makalla amesema hayo wakati wa kikao kazi maelekezo kilichojumuisha
Viongozi kuanzia ngazi ya Wilaya, Kata, Mitaa na Wadau mbalimbali wa
maendeleo ambapo amesema Jiji la Dar es salaam Lina uwezo wa kutoka
kwenye nafasi ya sita kwa Usafi Barani Africa na kushika nafasi za juu.
Ilikufanikisha
zoezi Hilo, RC Makalla ameelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi
kuhitisha kikao na Watendaji wa Kata na Mitaa kabla ya Julai 30 ili
kuweka mipango!kazi wa kufanikisha.
Aidha
RC Makalla ameelekeza pia Usafi wa Mito na maboresho ya Fukwe huku
akiwataka Wakandarasi wa uzoaji wa taka kuhakikisha taka zinazokusanywa
zinaondolewa kwa wakati.
Maelekezo
ya RC Makalla yamepokelewa kwa mikono miwili na Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi, Wastahiki Meya, Wenyeviti na Watendaji wa Kata/ Mitaa,
Wakandarasi wa taka na Wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo wameahidi
kuyatekeleza kwa ufanisi mkubwa.
Miongoni
mwa Barabara kubwa ambazo RC Makalla ameelekeza kufanyiwa Usafi wa Hali
ya juu ni Nyerere road, Bagamoyo road, Morogoro road, Mandela Road,
Kilwa road, Pugu Road na nyinginezo kwakuwa zinabeba taswira ya Jiji
Hilo.
No comments:
Post a Comment