HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2022

TIMU NANE KUSHIRIKI BONANZA LA SHIWATA

Na Mwandishi Wetu


MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa Bonanza la soka kwa maveterani kitakalofanyika uwanja wa Sigara, Tabata  Dar es Salaam Julai 8 mwaka huu.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Deogratius Kway alisema timu nane zimethibitisha kushiriki tamasha hilo litalitoa mshindi kwa njia ya mtoano.

Alizitaja timu hizo kuwa ni watetezi wa tamasha hilo Kitunda Veterani, wenyeji wa tamasha hilo Tabata Veterani. timu ya Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na TBC Warriors.

Mwenyekiti Deo alizitaja timu nyinginekuwa ni Machinga Complex veterani, Tabata Kisukuru veteran, Mchikichini Veterani na First Eleven ambapo mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapata zawadi ya fedha taslimu.

Alisema Bonanza hilo litaanza saa 3  asubuhi na mgeni rasmi atakuwa mkuu wa wilaya ya Ilala,Ngwilabuzu Lubigija atayefungua na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala atafunga.

No comments:

Post a Comment

Pages