Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Wamkele Mene (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (katikati), wakati alipotembelea banda hilo, katika ufunguzi rasmi wa maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji. (PICHA NA JOHN DANDE).
Mgeni Rasmi katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Wamkele Mene (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Sabasaba, Angelita Msaki, alipotembelea banda hilo, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Wamkele Mene (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la sabasaba, Angelita Msaki, alipotembelea banda hilo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayaendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Sabasaba, Angelita Msaki na Meneja wa Biashara wa Kanda ya Mashariki, George Yatera (katikati).
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda (kushoto) akizungumza na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la sabasaba, Angelita Msaki, wakati wa maandalizi ya kumkaribisha Mgeni Rasmi wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Wankele Mene, katika banda lao.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Stephen Adili (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Bwana akiyetembelea banda la Benki ya CRDB katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la sabasaba, Angelita Msaki.
No comments:
Post a Comment