Na Irene Mark
Taasisi ya Elimu Tanzania ( TET) imewaomba wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kutembelea katika banda lao lilipo Jakaya Kikwete kwenye maonesho ya 46 ya kitaifa ya kibiashara maarufu Sabasaba.
Ofisa Uhusiano wa TET, Angella Msangi amesema kuwa katika banda la TET wananchi wataweza kujionea machapisho mbalimbali yanayochapishwa na kufahamu kazi zinafanywa.
"Nawakaribisha katika banda letu,wananchi wataweza kuona kazi mbalimbali tunazofanya,” amesema Msangi.
Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28,2022 na yanatarajiwa kufungwa Julai 13, 2022.
No comments:
Post a Comment